SERI K
A L I i m e a h i d i kuendelea kuhakikisha mazingira ya kazi ya waandishi
yanaboreshwa na pale ambapo maisha yao yanakuwa hatarini, haitasita kuchunguza
na kuchukua hatua stahiki bila uoga wala upendeleo. Kauli hiyo ilitolewa na
Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa
Pili wa Mashauriano Kati ya Baraza la Habari na Wahariri wa Vyombo vya
Habari,mjini Tanga jana. a ihdiremii lakireSa mesilaa iPmpango wa kuendesha
shughuli za serikali kwa uwazi (OGP ) ambao unasimamiwa na wizara yake na
wamedhamiria kuhakikisha kuwa Sheria ya
Haki ya Kupata Habari inatungwa kwa
kuwashirikisha wadau wote ili kuwapa wananchi haki ya kutafuta habari na
kuzitumia kwa maendeleo yao. Alichukua nafasi hiyo kuwapa pole wanahabari na
wanandugu wa waand i s h i w a l i o p a t a madhara mbalimbali. “Napenda
kuwahakikishia kuwa Serikali iko pamoja nao na inatambua mchango mkubwa ambao
waandishi mnatoa katika kuleta maendeleo ya nchi yetu,” alisema na kuongeza;
“Mnayo haki na kwa hakika ni wajibu wenu kudai kwa sauti kubwa wale
walioshiriki katika kuwadhuru wanahabari watiwe nguvuni na kufikishwa katika
vyombo vya sheria.” Alisema waandishi wa habari wajiepushe na ushabiki wa aina
yeyote ile uwe wa kidini, kisiasa au kikabila kwa kutumia vyombo vya habari.
Alitoa pongezi kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kuona umuhimu na kuunda
Baraza . irabaHa ya insaTa la bitaKa lAlifafanua kuwa ni matumaini yake umoja
wao katika Baraza hilo utafanikisha masuala ya wanahabari kuingizwa katika
Katiba ijayo. “Naamini baadhi ya masuala hayo ni pamoja na lile la Uhuru wa
kupata habari, Uhuru wa vyombo vya habari na Uhuru wa uhariri pamoja na Uhuru
wa kujieleza na kutoa maoni,” alisema Waziri Chikawe. Alisema iwapo masuala
hayo yatasimamiwa kwa dhati yatapata nafasi katika Katiba mpya. “Na kama
ikitokea kwamba katika rasimu ya kwanza ya Katiba itakayotolewa hayatakuwepo
nyinyi, wenyewe kupitia Baraza lenu muyawakilishe mapendekezo hayo kwenye tume
ya mabadiliko ya katiba ili yaingizwe katika Katiba mpya,” alisisitiza.
No comments:
Post a Comment