Na Pendo Mtibuche,
Dodoma
MFUKO wa
Pensheni ya Mashirika ya Umma ( P P F ) umesema kuwa kwa muda wa siku tatu za
maonesho ya mifuko ya hifadhi ya jamii yanayofanyika mjini Dodoma chini ya
usimamizi wa Mamlaka ya mifuko hiyo (SSRA) umefanikiwa kutembelewa na wananchi
wapatao 572 na kupata elimu.
Akizungumza na gazeti hili katika viwanja
vya maonesho hayo vya Mwalimu Nyerere Square, Meneja wa Kanda ya Mashariki na
Kati, John Mwalisu alisema kuwa maonesho hayo ya mifuko ya hifadhi ya jamii
yamekuwa na manufaa makubwa kwa jamii ya mkoa
huo.
Alisema kuwa kwa muda wa siku tatu za
maonesho hayo mfuko wao wa PPF umefanikiwa kutembelewa na wananchi mbalimbali
wapatao 572 lakini pia wamefanikiwa kutoa taarifa zaidi ya 217 za michango ya
wanachama wao.
Mbali na hilo pia alisema kuwa
walifanikiwa pia hata kuandikisha wanachama wapya wakiwemo wabunge
ambaowameonesha kuufurahia mfuko wao na kuahidi kueneza ujumbe huo kwa wabunge
wengine.
Akizungumzia hali halisi ya mfuko huo
alisema upo katika hali nzuri kwani unaweza kulipa madeni yake na hata kubakiwa
na ziada na kueleza kuwa thamani ya mfuko huo kwa sasa ni sh. trilioni 1.09
lakini lengo lao hadi kufikia 2015 mfuko huo uwe na thamani ya sh.trilioni 2.
Akizungumzia suala la wanachama wa mfuko
huo kwa nchi nzima wanafika zaidi ya 218,000 ambapo kwa mwezi mfuko huo unatoa
zaidi ya bilioni tatu kwa ajili ya pensheni za wastaafu.
Kwa upande wake naye Ofisa Mwandamizi wa
uwekezaji katika mfuko huo, Anna Shayo akizungumzia hali halisi ya uwekezaji
katika mfuko huo alisema kuwa mfuko huo umewekeza katika mali zinazohamishika
na zisizohamishika.
Alisemakuwa wamefanikiwa kuwekeza katika
majengo ya kuishi, majengo ya biashara, hisa za makampuni wamefanikiwa kuwekeza
katik a vitegauchumi ambavyo riba zake zinajulikana kabla.
Kwa upande mwingine pia alisema kuwa
wamefanikiwa kuwekeza katika mikopo amb a p o kwa s e h emu wamefanikiwa
kujenga baadhi ya majengo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Ukumbi wa Bunge,
majengo mengine Arusha na hata kuwa na saccosza wanachama wa PPF 42 ambazo
wameshazikopesha bilioni 54 tangu mwaka 2004.
"Kwa upande wa saccosmwezi huu yaani
Mei tunakusudia kutoa bilioni moja nyingine kwa ajili ya kufungua
saccosnyingine mbili katika jiji la Dar es Salaam na hivyo tutakuwa na saccos44,
hayo ni mafanikio ya mfuko," alisema.
Kwa upande wake Ofisa uhusiano wa Mfuko
huo, Lulu Megele akizungumzia suala zima la wao kushiriki maonesho hayo alisema
kuwa mfuko wa pensheni wa PPF umeshiriki maonesho hayo lengo likiwa ni kutoa
elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko huo.
Alisema kuwa umuhimu wa wananchi kujiunga
na mfuko huo ni kutokana na kuwa na faida nyingi ambazo ni pamoja na kuwepo kwa
fao la uzee, ugonjwa, kifo, wategeneziu, elimu, kiinua mgongo na fao la
kujitoa.
Akizungumzia mafanikio ya mfuko huo
alisema kuwa umewezesha kuwasomesha zaidi ya watoto 1,333 katika shule za
msingi na sekondari katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Alisema kuwa mfuko huo ulifikia uamuzi wa
kuwasomesha watoto hao kutokana na kuwepo kwa tatizo kwa wasimamizi wa mirathi
pindi wazazi wa watoto hao wanapopoteza maisha.
Alisema kuwa hadi kufikia Desemba
mwaka jana jumla ya sh. milioni 682.9 zililipwa kama mahitaji mbalimbali kwa
wanafunzi hao.
No comments:
Post a Comment