Na Mwandishi Wetu,
Moshi
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri K u u y a Ta i f a
, (NEC) wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM), Bw. Jerry Silaa, amesema kukosoana
miongoni mwa viongozi ndani ya CCM na Serikali ni njia mojawapo ya kukiimarisha
chama hicho na isitafsiriwe vingine.
Bw. Silaa ambaye pia ni Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam, aliyasema hayo mjini
Moshi, mkoani Kilimanjaro, wakati wa hafla ya kuwapokea wanachama wapya 155 wa
CCM wa tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara, cha mjini Moshi,
(MUCCoBS).
"Ni vyema tukajenga tabia ya kukosoana pale
tunapoona
mwenzetu au wenzetu wamepotoka katika kutekeleza ilani ya chama chetu
la sivyo ahadi zetu kwa wananchi na malengo ya ilani yetu ya miaka mitano
hayatatimia," alisema na kuongeza kuwa makosa anayoyafanya mtu yawe ni ya
kwake na kuwajibika nayo
na si chama wala serikali.
Bw. S i l a a a l i s ema pia
haitakuwa vyema k u w a c h u k u l i a w a l e wanaojitolea kukikosoa chama au
serikali kama wasaliti na kwamba kwa kufanya hivyo itakuwa ni sawa na kubariki
mabaya ambayo yanakemewa.
"Wanaokosoa mapungufu katika
utekelezaji wa ilani yetu wasionekane kuwa ni wasaliti kwa kuwa kwa kufanya
hivyo tutakiangamiza chama chetu ambacho bado watu wana imani nacho,"
alionya.
Alitoa mwito kwa viongozi wa CCM
MUCCoBS , kuungana na wale wa Umoja wa Vijana wa CCM, (UVCCM), Mkoa wa
Kilimanjaro pamoja na wenzao wa mikoa mingine ili kuangalia uwezekano wa k uwa
s i l i s h a k e r o zinazohusiana na mapungufu yaliyoko katika bodi ya mikopo
kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu na changamoto zake ili kuzitafutia
ufumbuzi.
Awali katika risala yake, kaimu katibu wa
CCM MUCCoBS, Bw. David Warioba, alisema kuwa moja
inayowakabili
wanafunzi ni mikopo kwa ajili ya wanafunzi hasa wale wa diploma ambao wanataka
kuendelea na mafunzo katika ngazi ya shahada.
"Kuna wanafunzi zaidi ya 700 wa ngazi
ya diploma hapa MUCCoBS ambao wangependa kuendelea katika ngazi ya shahada,
lakini wanashindwa kutokana na serikali kupitia bodi ya mikopo kutoa kipaumbele
kwa wale waliotokea kidato cha sita," alisema.
Aidha alitoa wito kwa CCM kupitia Serikali
yake kuwachukulia hatua wale wote wanaotumia dhamana waliyopewa kujinufaisha
wenyewe jambo ambalo alisema limechangia watu kuinyooshea serikali kidole
pamoja na mambo mazuri ambayo imeyafanya na inayoendelea kuyafanya.
Kwa u p a n d e wa k e Mwenyekiti wa UVCCM
Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Frederick Mushi, alitoa wito kwa CCM na serikali yake
kuwatumia wasomi katika kutekeleza ilani yake.
SI NASIKIA VYAMA HAVITAKIWI KWENYE TAASISI ZA LEARNING HAO CCM SIO CHAMA?
ReplyDelete