MTOTO mwenye
umri wa miaka sita (pichani) amefariki papo hapo baada ya kuangukiwa na ubao
wenye misumari kichwani wakati akipita njia kuelekea shuleni na kusababisha
kupoteza maisha.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo jana, Kamanda wa Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema
tukio hilo lilitokea jana eneo la Ilala Bungoni, saa 12 asubuhi eneo la Mtaa wa
Mafuriko jijini Dar es Salaam.
Kamanda huyo alisema,
marehemu huyo Mariam Abdullah ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Alfurqan
iliyopo Buguruni Malapa aliangukiwa na ubao huo ulioangushwa na Oliva Isdori
(20).
M w a n a m k e
a m b a y e anajishughulisha na mamalishe ambaye ni mkazi wa
eneo hilo kwa
lengo la kujipatia kuni ili kupikia chakula.
"Saa 12
asubuhi kulikuwa na mtoto Mariam, alikuwa anakwenda shule...jirani yake
kulikuwa na ghorofa linajengwa ambapo juu ya hilo ghorofa kulikuwa na mama
mmoja alikuwa anaangusha mabaki ya mbao (kuni) kwa ajili ya kwenda kupikia,
sasa kwa uzembe wa mama huyo alikuwa anaangusha kuni hizo bila ya kuangalia
chini na kumpiga mtoto huyo kwa ubao wenye misumari kichwani na kusababisha
kifo chake," alisema Kamanda Minangi.
Alisema, mama
huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mauaji na kuongeza kuwa mtu anapofanya
uzembe na kusababisha kifo anawekwa katika kundi la wauaji.
Kamanda huyo
alisema, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi mara baada ya kukamilika kwa
uchunguzi ambapo sheria itafuata mkondo wake.
Kwa upande wake
mjumbe wa eneo hilo, Jumbe Magagula alisema tukio hilo lilitokea saa 12 asubuhi
wakati marehemu huyo akienda shuleni na kwa bahati mbaya ndipo mtoto huyo
alipatwa na mauti hayo.
"Jengo hili (ghorofa)
linamilikiwa na Benitho Thadei Chengula na aliyehusika na mauaji hayo ni
mfanyakazi wake,imekuwa ni kawaida yao kila siku asubuhi huwa mamalishe huyo
hupanda juu ya jengo hilo lenye ghorofa nne, kwa ajili ya kuchukua kuni, kwa
bahati mbaya leo (jana) binti huyo hakujua kama kuna mtoto anapita njia katika
eneo hilo,ndipo aliporusha ubao wenye misumari na kumpiga mtoto huyo kichwani
na kusababisha kifo chake," alisema.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya
Ilala, Edson Fungo aliwashutumu mafundi wa jengo hilo kwa kutofuata utaratibu
hali iliyopelekea kusababisha kifo cha mtoto huyo.
Gazeti hili lilimtafuta mmiliki wa
jengo hilo ambapo simu yake haikupatikana jambo lililopelekea kumtafuta katika
simu ya mkewe aliyejitambulisha kwa jina moja la Grace na kusema kuwa, mumewe
Chengula amesafiri na yeye yupo polisi kituo cha Pangani akishughulikia tukio
hilo.
Mhandisi wa Manispaa ya Ilala, Ogare
Salum alisema ametuma watu kufuatilia tukio hilo ili kupata taarifa kuhusiana
na mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kuupata ukweli.
Na y e Mama mz a z i wa marehemu
huyo, Maimuna Ibrahim(32) alisema anaiomba Serikali iwaangalie wananchi
wanyonge na kulihusisha tukio hilo ni kutokana na pesa za mmiliki wa jengo
hilo.
Kwa
upande wake mwalimu mkuu wa shule alipokuwa akisoma marehemu huyo, Mwalimu
Abdallah alisema tukio hilo wamelipokea kwa masikitiko makubwa kwani mwanafunzi
huyo alikuwa kinara darasani kwa kufanya vizuri katika masomo yake ikiwa ni
pamoja na tabia njema na nidhamu kwa walimu wake.
No comments:
Post a Comment