05 April 2013
Nape afichua siri za CHADEMA *Akanusha tuhuma dhidi ya CCM, Mwakyembe *Adai chama hicho sasa kinatumiwa na mafisadi
Na Gladness Mboma
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema tuhuma zinazotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), dhidi ya chama tawala ni matokeo ya chama hicho kulishwa uongo na
mafisadi wanaotaka kushika dola kwa gharama yoyote.
Alisema madai ya CHADEMA kuwa Kampuni ya Chama cha Jitegemee Trading Company, inayomilikiwa na CCM kuingia mkataba na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kwenye mradi wa umanuzi wa bandari kavu kwenye eneo la SUKITA,
hazina ukweli wowote.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi,
Bw. Nape Nnauye, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya madai hayo.
Alisema eneo la SUKITA ni mali ya CCM lakini PTA na Jitemegee, hawajaingia mkataba wowote kama inavyodaiwa na CHADEMA kupitia gazeti moja linalotoka kila siku (si Majira), kuwa kampuni hiyo imepewa zabuni ya kupanua bandari kavu.
Bw. Nape alisema, gazeti hilo limemnukuu Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa CHADEMA, Bw. Benson Kigaila, ambaye aliishutumu Wizara ya Uchukuzi na Waziri wake Dkt. Harrison Mwakyembe, akidai kiongozi huyo amekiuka taratibu
na kutoa zabuni ya upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam kwa
CCM kinyume na taratibu za manunuzi.
“Eneo la SUKITA limeombwa na wawekezaji wengi wakiwemo TPA, masharti waliyopewa waombaji wote ni kuleta mapendekezo ya mipango yao ya kibiashara kabla ya kufikia uamuzi wa nani anayewekeza kwa ubia na Jitegemee katika eneo hilo.
Alisema CHADEMA wanapitia wakati mgumu kisiasa kwa kuanza kuvuna walichopanda muda mrefu katika siasa za nchi, kukosa uwezo wa kufikiri na kushindwa kutofautisha barua ya maombi
ya ushirikiano ili kuendeleza eneo la SUKITA na mkataba.
“Wanacholalamikia CHADEMA ni barua ya TPA kwenda Jitegemee wakiomba ridhaa ya kushirikiana ili kuliendeleza eneo la kampuni lenye ukubwa wa zaidi ya ekta 100 katika mfumo wa ushirikiano ambao ni wa kawaida kwani unafuata taratibu na sheria zote.
“Jitegemee imekuwa ikitekeleza shughuli za uwekezaji muda
mrefu kwa kufuata taratibu zote za sheria na nchi kwa ujumla,
CCM inatambua tabia ya viongozi wa CHADEMA kudandia
kila gari linalopita bila kujua linakokwenda kwa kugeuza kila kinachofanyika nchini ili mradi hakifanywi na wao,” alisema.
Aliongeza kuwa, CHADEMA kina uwezo mkubwa wa kutunga
uongo na kupanga machafuko na ndio sababu ya Watanzania kuwakataa kila kukicha na chama hicho kufa kwani njia ya
muongo ni fupi.
“Tunazo taarifa kuwa uongo huu wamelishwa na baadhi ya mafisadi waliotaka kutumia eneo hili la CCM kujaribu kukaa katikati ya mwekezaji yeyote ambaye atajitokeza na Jitegemee ili waweze
kujinufaisha kwa masilahi binafsi.
“Huu ni mwendelezo wa CHADEMA kutumiwa na mafisadi katika mambo yao, Watanzania tuwapuuze na kuwaepuka, umbumbumbu wa iina hii unatia mashaka juu ya uwezo wao wa kufikiri na kupambanua mambo,” alisema Bw. Nnauye.
Alisema CCM inatambua na kumpongeza Dkt. Mwakyembe na Wizara yake kwa kazi nzuri ya kuongeza ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam hivyo wasikatishwe tamaa na mafisadi wachache.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
CHADEMA KINA UPUNGUFU MKUBWA WA RASILIMALI WATU ILIDHIHIRIKA PALE WALIPOTOA BUDGET MBADALA AMBAYO ILIONEKANA KICHEKESHO WAJIPANGE KWA HATUA ZIFUATAZO KUFANYA UCHAGUZI ILI WA CHAMA KUANZIA MONEY HADI NGAZI YA TAIFA ILI KUPATA RASILIMALIWATU INAYOWEZA KUKABIDHIWA DOLA ILIYOKO NI CHOKA MBAYA NI SAWA NA KUMNYANGANYA CHONGO USUKANI ASIENDESHE GARI UKAMPA KIPOFU AENDESHE GARI HILO LA ABIRIA LITAISHIA KUZIMU
ReplyDeleteNA ccm MAGAMBA WAO WANARASILIMALI WATU WENGI WANAOLIPELEKA TAIFA MKENGE KWA KUSAINI MIKATABA MIBOVU,UFISADI,NA KUSAINI MIKATABA BAA ,NA KUPOLOMOSHA ELIMU YA WATOTO WA KITANZANIA,NA KUUZA TWIGA QATAR NA KUFUKUZA WAMASAI NGORONGORO NA KUWAPA WARABU VITALU HIYO NDIO RASILIMALI UNAJIVUNIA HUKO ccm.
DeleteMara nyingi wenye akili mgando wanaona CHADEMA kwani hayo ya ccm una uhakika gani kama ni kweli kiasi useme CHADEMA ni waongo. Acheni ushabiki zungumzeni jinsi ya kutatua matatizo na kero za wananchi CHADEMA ni wakweli daima.
DeleteChadema wakweli daima? Unajua vizuri background zao. Hao hawalilii ziki wanalilia madara tuuu! Kama unafikiri watatatua njaa yako hapo umenoa. Hebu waulize wamefanya nini katika majimbo yao zaidi ya kuikosoa serikali kwa sauti kubwa.
Deletechadema wamefunga akili zao. WamepÄnua midomo yao.Hatari
Deletemmimi naona ccm ndo mafisadi wakubwa wanaokula fedha za umma na bila kujali wananchi masikini chadema wanajitaidi kufichua maovu ya ccm bila ya hayo fedhaa za uswisi mpaka leo kinacho endelea wajua zitto kapeleka ushaidi wamekaa kimya c wana ccm ndo wako huko haitoshi leo nauli zimepanda kupandisha nauli i namaana hata chakula au mfumuko wa bei za vyakula utapanda angali wananchi wako bado kwenye hali ya umasikini mishahara midogo je wananchi wa kawaida watayamudu maishahayo?usiwe unandika kutetea ujinga tu yamkini umeandika angalia maisha halisi ndipo uandikwe BWEGE WEWE
ReplyDeleteJamani hapa hatutukanani, tunaelimishana tu matusi ya nini,kwa mtu mwenye hekima na busara huwezi kumtusi mwenzio. Lets share ideas and not insulting each other, it's awful!!!
Delete2015 ndio mwamuzi wa yote
DeleteSerikali isiwe na upendeleo, linapokuja swala la ardhi, iwe kama linavyofanyika kwa watu wengine. Kwa nini eneo la SUKITA, eti kuchukuliwa na TPA, iwe kwenye mkataba, wakati wapo wananchi wengine ambao maeneo yao, aidha yamechukuliwa tu na Serikali, au kulipwa fidia? Hilo eneo la SUKITA, kama ni kwa maendeleo ya nchi, lichukuliwe tu na kuendelezwa, na kama kweli CCM walililipia, basi na wao walipwe tu fidia na si kuingizwa kwenye mkataba.
ReplyDeleteMwakyembe anafanya kazi yake kama inavyotakiwa na katika utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi, anamsaidia Rais katika kutekeleza ahadi za uchaguzi na tunajua rekodi yake ya utendaji kuwa haina madoa.
ReplyDeleteHivi karibuni kumekuwa na mafisadi ambao wanajaribu kuwapaka matope kwa gharama yoyote ile watu ambao wana nia njema na nchi yetu. Na pia kujaribu kuwasafisha baadhi ya watu ambao wanajulikana kwa jinsi walivyoliingiza taifa hili katika umasikini na leo hii wanadhihirisha wazi bila kificho jinsi walivyojinufaisha.
Mwakyembe tunakushukru sana kwa kazi unayofanya kwa manufaa ya wananchi na si vinginevyo.
Wewe unayesema waziri Mwakyembe anafanya kazi nzuri unajidanganya kwa kuwa na yeye ni nguvu ya soda kama wenzake waliotangulia yaana waziri Magufuli na Prof.Tibaijuka.Muulize waziri wako unayemsifu Mwakyembe amawafukuza mafisadi bandari mpaka leo ni zaidi ya miezi 3 mafaili yao yako kwa DPP ua chini ya uvungu wa kitanda cha CCM.Nipe jibu.
Deletekwani hayo mafisadi ni ya chama gani?
Deleteni yale ya CCM ambayo yalisemwa ni magamba halafu yakawa si magamba halafu yakawa maviongozi na matajiri makubwa yasiyoguswa na sheria. uko hapo wewe maskini?
Deletejamani zungumzeni kwa hoja ccm imeshindwa 1.elimu imeshuka wakati wa mkapa ilikuwa 63% awamu ya nne ni asilimia 34%. mbili 2.huduma za afya ni mbaya kwa kiwango kikubwa nchini.3.ubadhirifu katika halmashauri za wilaya umejikita mizizi watumishi wanaiba fedha za miradi mbalimali ya afya,kilimo,elimu,n.k nne 4.kashfa za kagoda,meremeta,richmond,radder,kiwira na north mara. sasa CHADEMA wanakosoa na kuikumbusha serikali kuwajibika kuwatumikia wananchi,sote tunajua jukumu la serikali ni kuwaondolea wananchi wake umasikini hivyo upinzani unakosoa ubaya unaofanywa na watumishi wa serikali kudhoofisha maendeleo ya taifa na wananchi kupambana na ufisadi na vibaraka wanaohujumu taifa hili,kwasababu Tanzania ni yetu sote sio ya ccm peke yake watu wanapaswa kuelewa hivyo.
DeleteTunakubaliana sasa kuwa nguvu ya pesa ya ufisadi inafanya kazi kuwachafua watu na viongozi wenye nia njema katika nchi yetu, bila shaka watanzania tunajua rekodi ya utendaji mzuri wa Mwakyembe.
ReplyDeletePia hata Nape anakili kuwa kuna baadhi ya watu baada ya kutekeleza sera za chama kwa kumsidia rais kutekeleza ilani y uchaguzi, wanatumia nguvu na pesa nyingi ambazo hazijulikani zinatoka wapi katika kujitafutia umaarufu na kuwachafua watendaji wazuri.
Watanzania tunatakiwa kuwa makini sana na watu wa namna hii, kwani lazima tukiulize pesa hizi wametoa wapi na wao ni waajiriwa au wawakilishi serikalini?, na je wana nia gani na watazirudisha vipi?
Mwakyembe tunakushukru sana na fanya kazi yako kwa manufaa ya nchi na wananchi, na umeonyesha kwa vitendo jinsi unavysaidiana na rais katika utendaji.
CCM tumewachoka na ufisadi wenu kila kukicha mnabuni jinsi gani mzidi kutuibia mnajiona kua nyie ndo wema kumbe nyie ndo mafisadi wakubwa mnajilimbikizia mali za wananchi tena bila hata ya uruma,mnafelisha watoto makusudi ili muendelee kututawala watoto wenu munawasomesha nje ya tanzania ila mwisho wenu utafika tu.bora CHADEMA wanawafumbua wananchi macho sasa mnacholalamika nini,achaeni ufisadi wenu na kusaini mikataba feki mkiwa baa hamna huruma na wananchi wenu.
ReplyDeleteMABILIONI YA SUKITA YALIYOPELEKWA LART KUTOKA NBC YALIISHIA WAPI? MAGARI YA CCM YANATUMIA MAFUTA KUTOKA SERIKALINI UKIGOMA WANAKUZUSHIA UCHADEMA
ReplyDeleteNAPE chama chako ovyo acha kujigamba
ReplyDeleteI hate CCM than anything. CCM ndiyo chanzo cha matatizo yote ya Watanzania. Ukombozi wa Watanzania ni lazima uanzie na kuiondoa CCM. Lakini Watanzania ni budi wajue ni rahisi kumwondoa madarakani kiongozi mzuri kuliko kiongozi mbaya. CCM haiwezi kuondoka kiurahisi kwa sababu ni kiongozi mbaya. Kiongozi mbaya huogopa kuondoka madarakani kwa sababu ya hofu juu ya nini kitafanyika juu yake baada ya kuondoka
ReplyDeletewewe Nape na chama chako hamna lolote, mmeshindwa kuongoza nchi. Nchi mnaongoza KIBUBUSA tafuta maana ya hii neno utajua, ccm nn bwana kwisha habari yenu, mnatumia mbinu nyingi wapi. Nani asiejua kuwa mnatumia rasilimali zetu kwa chama chenu!!! nani asie jua kuwa chama chenu hakina dira wala mwelekeo!! kolimba aliwaambia nyinyi, nendeni zenu bwana
ReplyDeleteAma kweli ccm imechimbia kaburi yenyewe kwa kupanua elimu na kuwapeleka shule. Sasa chadema ichapishe minoti mpate ajira mtulize munkari kidogo. Mnatetea wakulima amabapo jembe mnalikwepa kama ukoma!!! Wasomi nyie na laptop zenu!
Deleteni kweli pamoja na matatizo yote, kuindoa ccm madarakani ni shughuli pevu na imegundulika mfumo wa elimu ukiboreshwa Tanzania, mabadiliko yatakuwepo na mabadiliko yanayotabiriwa ni ccm kung'oka na kupisha wengine. lakini wameshazisoma dalili. na pengine kufelisha watanzania yawezekana ni mkakati wa makusudi ili kupunguza spidi ya mabadiliko ili kukinusuru chama ambacho hakijajiandaa kuongoza wasomi wazuri waliokosa ajiri. nape unafaa na unapiga debe kitaalumu, japo gari lenu bovu hata kwa mwonekano lakini abiria wanajaa, namshauri tajiri asikuache na akupromote uwe dereva badala ya kubaki kuwa konda.
ReplyDeleteda minadhani ni wakati sahihi kwa watanzania kujua nini ccm inafanya juu ya watanzania wa leo na wajao,ukweli wananchi tumechoshwa na majigambo ya wanasiasa uchwala kama NAPE,watanzania tuamke na tusonge mbele tuachane na maneno ya wanasiasa hawa,CHADEMA ni chama makini na chenye lengo la kuwakomboa watanzania masikini walio wengi ndani ya nchi hii.CCM hamuna jipya by now,twawaomba kaeni pembeni sasa,ni dhamu ya CHADEMA.
ReplyDeleteCCM ni chaka la majambazi. Yeyote aliyemo hata awe Mwakyembe, Magufuli au Tibaijuka ni wale wale. Waingereza husema show me your friends I will tell you who you are. Tatizo la watanzania ni kupenda kujikomba na kutathmini mambo kwa uoni mfupi. Leo utasikia watu wasikesema eti Kikwete anaangushwa na watendaji wake kwa mfano wakati yeye ndiye muungu wa Ufisadi tangu alipoiba pesa ya EPA ya kuhongea watanzania. Tunachopaswa kufanya watanzania tunaopenda nchi yetu na mstakabali wake ni kuwatolea uvivu hawa majambazi . Tuingie mitaani tufanye walichofanya walibya walipomkamata na kumuua Gaddafi. Siku nikiona Kikwete na genge lake wakilia kama Gaddafi nitafurahi sina mfano. Hata nikifa baada ya siku hiyo nitakuwa nimeishi na kufa kwa heshima vinginevyo tunaendelea kuzebeza bila sababu
ReplyDeleteshow me your friends I will tell you who you are. nimeipenda. CCM jamani????? SIKUPENDI!!!!!!
ReplyDeleteNIKIFA LEO NIKIKUTA HUKO CCM NI CHAMA TAWALA HALAFU NIKAULIZWA CHAGUA KUJIUNGA NA CCM AU RUDI ULIKOTOKA JAWABU NI KURUDI NILIKOTOKA BILA KUMUMUNYA ULIMI. KUDADADEKI. KUDADADEKI NI NENO RASMI LINALOTUMIKA BUNGENI TANZANIA NA WABUNGE WATUKUTU WA CCM.
Chama tawala halahala mti na jicho
ReplyDeleteHuko chadema kuna wasafi gani hao waliokuwa mapandri upadri ukawashinda kwasababu ya uchafu? Hao waliokuwa madisco jokker na sasa wanaongoza chama ndiyo tuwape nchi? Hakuna safu ya maana ya uongozi chadema na mwisho wenu uko karibu. uongozi hautafutwi kwa nguvu bali kwa sera safi zitakazotukomboa
ReplyDeleteMnarumbana weeeee! lakini mwisho ndio mnawapa maaarifa ili wajue mmewajua kwa upande upi na waanze kuwala tena kwa upande mwingine, kwahyo marumbano yenu mnawafaidisha Mafisadi
ReplyDeletekelele za nape juu ya operation vua gamba iko wapi? kama nape ni mkweli atutajie hayo magamba ni kina nani na kwa nini amebadili wimbo. nape anaongozwa na tumbo lake msimsikilize ni bora aongee lugola wa mwibara.
ReplyDeleteDisco dancer msafi? kaiba hela benki kuu nani hajui?
ReplyDeletemambo ya kuongoza nchi ni tofauti na kuongoza night clab.
ReplyDeleteCCM NI CHAMA KIKUBWA, CHADEMA NYINYI NI WATOTO WADIGO SANA MSIPENDE KUSHINDANA NA CCM SIO SAIZI YENU, AU HAMJUI HESABU? HESABUNI WABUNGE WENU MGAWANYE NA WA CCM, NA MADIWANI WENU, SISIMIZI ANASHINDANA NA TEMBO? MAAJABU HAYA?
ReplyDeleteHebu jaribu kuongea kitu cha msingi, achana na hayo mashairi, hayakusaidii lolote, Ukweli utabaki palepale hata kama utaki
DeleteCHADEMA SIZI YAKE NI NCCR, CUF, TLP NA WENGINE. MSIPENDE KUJIKUZA KUSHINDANA NA CCM. MTAPASUKA MSAMBA? SHAURI YENU?
ReplyDeleteCCM NI MAFIA WOTE ,MIZIZI YAO IMETANDAA KAMA MAGUGU,KA UNAITETEA AIDHA HUJUI ULIFANYALO,AU NA WEWE NI MAFIA,KAMA SIO UNA HISA FULANI NAO.I JUST HATE CMM MORE THAN ANYTHING.ONE DAY TZ WILL REBORN AGAIN!
ReplyDeleteUZURI HUKOMENTI KWA MBO YA UCHUMI NA YA KIJAMII. HATA KAMA MTOTO KABAKWA NA MTU MZIMA SIONI KOMENTI YOYOTE, HATA KAMA KUNA HISA AMA AJIRA IMETANGAZWA SIONI LOLOTE. NJOO KWENYE SIASA HASA YA CHADEMA NDIPO UTAONA CHADEMA WANYOJUA KUCHONGA. UTAFIKIRI WOTE WANA SHAHADA ZA SIASA. SOMENI MAMBO MENGINE MTAJUA NCHI HII INA WASOMI WA KUAMINIKA. MUTOE MAONI YA KUJENGA NA KUWASIDIA ZAIDI. MAFISADI WAKO NA WAMEJIFICHA KAITIKA KILA CHAMA. VIONGOZI WAZURI PIA WAKO KATIKA KILA CHAMA. WAACHIENI WANANCHI WAAMUE MISIWATISHE. KWAHIYO KAMA BABA YAKO CCM HUKO KIJIJINI NAYE TUMWITE MAFIA?
Deletedude i am not talking about chadema ,i am not even in a country.I am talking about MAFIA ccm.I don't even care about chadema or whatever' for me is the situation people are living in by now.I am sorry if I offended you dude .And I doubt my parents to be in politics all they care is church.
ReplyDeleteYou very goood person you know. When you talk about the ruling part, you talk about many people but when is all about these tiny seasonal political parties, you talk about few unique personalities, and few privillaged students who demand for better allowances. Of which is their right to do so. But it should never interefer with the national security, whose costs you will never be able to bear. Other countries sick refuge in Tanzania. But Tanzanian have no where to go as the whole African continent is in verge of war or serious social unrest. We are more democratic and our leader are ready to be insulted even by a little boy without causing much trabble. We have periodical elections. We have an examples of pairs os top leaders who relingushed their power and are peaceful retirement. Many ex-ministers have come back to ordary citizens without caos. It is even than the USA. So think twice when you make any serious allegetions. Otherwise you will invite to power people who wll never be ready to get out. Then you will regert and see who is real MAFIA.
DeleteWhat you shared is absolutely true. we need sensible ideal sharing like this!!!
Deleteni vigumu sana kuondoa usemi wa kwamba "samaki mmoja akioza ni wote wameoza",wapo watendaji wazuri sana ndani ya CCM ila kutokana na wachafu wachache ambao wenyewe wanawaficha kwa masilahi ya chama basi nitatizo,kwa zama kama hizi ambazo akili nyingi zinatumika ni vigumu kuwapa madalaka watu wenye upeo kama wa Nnauye ambao wanazani ukada wa vyama ndo utaleta maendeleo ya taifa hili masikini,Tatizo sio CCM tatizo ni wanaCCM hasa wale wanaodhani kwamba taifa hili watu wake watakuwa vipofu wa maono milele,.CHADEMA kama wapinzani wanafanya kazi yai kama wapinzani siku zote "lisemwalo lipo kama halipo...................."
ReplyDeleteumeongea ukweli best ,wapo watu wapiga kazi na niwakweli kabisa.ila wamezungukwa na hao wabaya hat wakiongea wanaondolewa quick.hapo ndio nawahesabia ni mafia .lazima system nzima isafishwe ile mizizi ya kimafya iondolewe.inatia uchungu unavyoona watu wanasuffer kiwango kile.na hawataki kuondoka wanajua siri zao zitakuwa open na haapo ndio wanaanza umafia.so it is not about chadema or ccm ,is about finding the right way people.
ReplyDeleteThank you so much for your reply, I know its not CHADEMA or CCM, here its depend the leadeship and their relationship with otheirs. I know according to that both of them they have no time with God,they just doing things for their benefit without thinking other people with their communities, Please tell them to pray to God. thank you.
Deletenape tushakuzoea,propaganda ndo ishu zako,sababu tu chama chako kipo madarakani ndo unatumia huo mwanya mda mwingine kuongea kashfa hadharani kuhusu chadema,HAUTUPI SHIDA,mbwa ukishamjua jina hakung'ati!!!!!!!
ReplyDeletePropaganda za Nape Mnyakule....! Siipendi CCM! Ingawa mm naishi nje ya nchi lkn naomba kila siku ccm itolewe madarakani ili tuone mwelekeo mzuri wa nchi yetu yenye rasmali nyingi na watu wengi sana maskini!
ReplyDeleteHee rasmali nyingi! Tuone mwelekeo mzuri wenye kuletwa na nani? Heri hata CAFU ina watu sio hao vijana mayoweyowe wa chadema. Kuna mmja alipata ubunge hivi karibuni kazi yake kuporomosha majengo tuuuuu!!!! Kuna mwingine kazi kuitisha maandamano tuuu! Kuna mwingine kazi kulialia tuuu! Jamani muwe makini. Kila mtu anataka mabadiliko lakini lazima ufukirie mabadiliko gani unayotaka. Kama ni muuza mitumba hujasoma hutawekwa hospitali kutibu watu. Kinachotakiwa ni kujengewa mazingira boara ya kuendeleza shughuli yako!!
ReplyDeleteWakati chadema iko bize na M4C ccm wako bize kutembelea vikundi vya vijana vya maendeleo. Vijana hao wenzenu wasio na kazi wakikimbia ovyo barabarani na kujaribu kuharibu mali za watu na kusimamisha shughuli za maendeleo, nyie wangojeni wakati wa uchaguzi, kwavile hata hawapigi kura. Wanawacheka kuvaa tisheti za kijani, wakati wao wanarubuniwa kwa makopo ya mbege na ugoro wa kizungu!
ReplyDeletehuku duniani kila mtuu anavutia kwake hata ww ukipewa kula lazima usikumbuke wananchi kama ulivyo aidi kwahiyo kila mtu anataka kuingia madarakani kwajili kuna kula kuzuri ukisha mpa mtu uwongozi kaa kushoto ule msoto wako mwenyewe kama niadsa ya watoto ya shule angaila mwenyewe alini hakuna atakaye kusaidia jipangeni na hata masilala mike maana kila mtu atanya yake atakapo kuwa kashika madaraka kwahiyo fanyeni kazi sana acheni lawama mkingojea serikali kila kitu iwaangalie mtakufa kama kuku wenye videri kikubwa tusome kisha tujiajiri tusingoje kuajiriwa tutasota kila mtu sikihizi nimsomi lol.............
ReplyDelete