WALIOKUWA wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ma z i n g
i r a ( N EMC ) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
kwa tuhuma za kushawishi rushwa ya sh.milioni 6.
Washtakiwa hao
ni Jerome Kayombo (33) na Milton Mponda (32).
Mbele ya Hakimu
Gane Dudu, wakili wa serikali kutoka Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU), Kelvin Murusuri alidai kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo kati
ya Mei 4 na 5, 2012 katika Kiwanda cha Kamal Steels eneo la Chang'ombe.
Alidai kuwa,
washtakiwa hao wakiwa kama maofisa ma z i n g i r a wa NEMC walishawishi wapewe
rushwa ya sh. milioni 6 kutoka kwa Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Sammer Gupta
ili iwe k ama k i s h awi s h i kwa Mkurugenzi huyo asiadhibiwe kwa kukiuka
sheria ya utunzaji mazingira.
Hata hivyo
washtakiwa hao walikana kutenda makosa hayo ambapo upande wa mashtaka ulidai
kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.
A i d h a , k e
s i h i y o imeahirishwa hadi Mei 23, mwaka huu itakaposikilizwa.
Washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana
baada ya kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya sh.
milioni 5 kila mmoja.
No comments:
Post a Comment