kAMPUNI
za kufua umeme kutoka nchini Sweden, zipo katika mchakato wa kuzalisha umeme
kwenye vyanzo mbalimbali baada ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kutokidhi
hitaji la kutoa huduma hiyo kwa wananchi wengi.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akiwakaribisha
wawekezaji hao na kuongeza kuwa, lengo la Serikali ni
kuiboresha TANESCO ili
iweze kutoa huduma bora.
Alisema tangu kuanzishwa kwa shirika hilo
mwaka 1961 ni asilimia 21 tu ya Watanzania waliopo mijini na asilimia saba
waliopo vijijini ambao ndiyo wanaopata huduma ya umeme.
“Kimsingi hali hii inasikitisha,
tumegundua kuwa TANESCO peke yao hawawezi kutoa huduma ya umeme kwa Watanzania
wenye hitaji hilo hivyo wataendelea kuumia,” alisema.
Prof. Muhongo aliongeza kuwa,
Serikali imewakaribisha wawekezaji hao kwa sababu haina fedha za kuwekeza
katika sekta ya nishati ili kusambaza huduma ya umeme.
“Pato la Taifa ni dola za Marekani
bilioni 28 ambazo tukizigawa, kila Mtanzania atapata sh. 6,000 hivyo lazima
tutegemee wawekezaji ili tuweze kujikomboa,” alisema.
Alisema wawekezaji hao mbali ya
kufua umeme nchini, pia watatekeleza miradi mbalimbali, k u b o r e s h a mi u
n d omb i n u , kusambaza umeme vijijini na kupunguza upotevu wa umeme.
Aliongeza kuwa, vyanzo vyote vya
umeme nchini vingeweza kuzalisha umeme wa megawati 1,438.24 lakini miundombinu
iliyopo hata kama umeme huo ungezalishwa, wangeshindwa kuusambaza kutokana na
ubovu wa miundombinu ambao hupoteza asilimia 23.4 ya umeme.
Alisema kampuni hizo zitafua umeme
kupitia upepo, miamba, kinyesi cha wanyama, maji, jua na kusisitiza kuwa ni
ndoto ya mchana kuitegemea TANESCO izalishe umeme kupitia vyanzo hivyo.
Kwa upande wake, Balozi wa Sweden nchini, Bw. Gunnar Oom, alisema
wameamua kuwekeza Tanzania baada ya kuona misaada pekee wanayotoa haiwezi
kuongeza
kasi ya maendeleo.
Alisema kupitia uwekezaji huo,
utasaidia kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kiuchumi pamoja na kubadilishana
uzoefu.
“Kupitia uwekezaji huu, pia
utasaidia kubadilishana bidhaa kwa kununua zilizopo Tanzania kwani nchi nyingi
za Afrika zinategemea sana kuuza mafuta, madini na mazao ya chakula nje,” alisema.
No comments:
Post a Comment