RAIS Jakaya Kikwete, amewapandisha vyeo
baadhi ya maofisa wa polisi akiwemo Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Michael
Kamuhanda, kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), na Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, uteuzi ambao unaanza mara moja.
Katika uteuzi huo, Kamanda Kova na
Isaya Mngulu, wote wamekuwa Makamishna wa Polisi (CP).
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, ilisema maofisa wengine waliopandishwa
vyeo katika ngazi hiyo ni Thobias Andengenye na Simon Sirro.
Msemaji wa
Wizara hiyo, Bw. Isaac Namtanga, aliwataja maofisa wengine kuwa ni Elice
Mapunda, Brown Lekey, Hamdani Omar Makame, Kenneth Kasseke, Abulrahman Kaniki,
Adrian Magayane, Sospeter Kondela na Ernest Mangu. Wengine ni
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, Hussein Laisseri,
Anthony Mwami, Adolfina Chialo, Mpinga Gyumi, Ally Mlege, Hezron Gyimbi na
Jonas Mugenzi ambao kabla ya uteuzi huo walikuwa Makamishna Wasaidizi
Waandamizi wa Polisi.
No comments:
Post a Comment