KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), imemteua Mattar Sarahan Said, kuwa mgombea wake wa chama hicho
katika Jimbo la Chambani, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba.
Uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao
cha siku moja kilichofanyika mjini Dodoma jana chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa,
Rais Jakaya Kikwete.
Pia chama hicho kimewateua Mjumbe wa
Kamati Kuu ya CCM, Balozi Seif Idd na Mwenyekiti mstaafu wa CCM ambaye pia ni
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi, kufunga kampeni hizo.
No comments:
Post a Comment