Na Mwajuma Juma,
Zanzibar
WAKUL IMA wa mashamba ya karafuu w ame s h a u r i w a kuzingatia ushauri
unaotolewa na wataalamu wa kilimo hicho ili kujenga nguvu za uzalishaji wa
uhakika wa zao la karafuu nchini.
Ushauri huo ulitolewa na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati wa ziara yake ya kukagua
baadhi ya mashamba ya Serikali ya miti ya mikarafuu ambayo yako chini ya
usimamizi wa baadhi ya wakulima ndani ya Mkoa wa Kusini Pemba.
Alisema kumejengeka dhana kwa baadhi
ya wakulima wa mikarafuu kujilimbikizia miti mingi ya zao hilo wakiwa na fikra
za kupata uzalishaji mkubwa zaidi jambo ambalo ni
ndoto kitaalamu.
Aidha, alisema kuwa Serikali
inaendelea na mikakati ya kuimarisha zao hilo na kuwasihi wananchi pamoja na
wakulima wa kilimo hicho kuunga mkono juhudi hizo, ambazo zimeleta faraja kwa
Serikali.
"Hivi sasa tunapaswa kuwa
makini katika uzalishaji wa zao la karafuu kitaalamu kwani wakati wa kuvuna
karafuu mpeta umepitwa na wakati kulingana na mazingira yaliyopo ya soko la
dunia," alisisitiza Balozi Seif.
Kwa upande wao wakulima hao
walieleza kuwa ufinyu wa taaluma ya kilimo hicho ndio uliokuwa ukiwapa ukaidi
na kupelekea kuleta mgongano kati yao na wataalamu wa kilimo hicho.
Mapema
Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Pemba, Hemed Salum
alisema kasi ya wakulima wa mikarafuu k u j i t o k e z a k u f y e k e a
mashamba yanayomilikiwa na Serikali hivi sasa imeongezeka zaidi.
No comments:
Post a Comment