ASKOFU Mkuu wa
Kanisa Katoriki, Jimbo Kuu la Songea, mkoani Ruvuma ambaye juzi ametangaza
kujiuzulu, Norbert Mtega, ameelezea sababu zilizomfanya achukue uamuzi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema hali
hiyo inatokana na kusumbuliwa na magonjwa mbalimbali ambayo ni presha, miguu,
magoti kujaa maji na kukosa usingizi kwa muda mrefu hivyo kujisikia
kizunguzungu na tayari amewahi kuanguka zaidi ya mara nne.
Alisema jamii inayomtazama inamuona
yupo kawaida lakini ana matatizo makubwa ya kiafya kwa muda mrefu ila alikuwa
akijitahidi kufanya kazi za kitume hali ambayo imechangia afya yake kuendelea
kuwa dhoofu.
Aliongeza kuwa, tatizo la afya yake
ni la muda mrefu hivyo ni bora astaafu mapema kabla ya kupoteza kumbukumbu ili
aweze kumpa Baba Mtakatifu muda wa kutafuta Askofu mwingine ambaye ataweza
kuongoza jimbo hilo.
“Nimeamua kujiuzulu kwa manufaa ya
Wakatoliki wote, Jimbo Kuu la Songea na jamii kwa ujumla ili niweze kupatiwa
matibabu kwani nikiendelea kung’ang’ania uongozi, hasara yake ni kubwa sana kwa
jamii ninayoiongoza.
“Namuomba Mungu anipe afya njema ili
niweze kutoa ushauri zaidi kwa waumini, Mapadri na Serikali,” alisema.
Amewahimiza waumini na viongozi wa
dini, kuendelea kuwa na ushirikiano, kuacha tofauti za ukabila ambazo
zinachangia kurudisha nyuma maendeleo ya Mkoa huo kwani ukabila ni hatari na
unaweza kuwagawa, kukwamisha maendeleo.
Alisema yeye anatambua kuwa, watu
wengi wameshtuka kutokana na uamuzi aliochukua hasa kwa kuzingatia kuwa,
alikuwa akifanya kazi zake bila wasiwasi.
Amemtaka Askofu ajaye, kuhakikisha
anaendeleza mema aliyoanzisha hususani katika nyanja ya elimu, afya, maji,
mazingira ili kuwaletea wananchi maendeleo na kuahidi kuendelea kutoa
ushirikiano na ushauri.
Mkazi wa Mkoa huo, Watson Nganiwa,
alisema Mtega atakumbukwa kutokana na kuwajengea uwezo wananchi wa j i t e g
eme e n a k u a c h a kutegemea wafadhili, kuhimiza wafanye kazi kwa bidii si
kutegemea misaada.
Alikuwa akishiriki shughuli mbalimbali za kijamii, kiserikali
na kuwashirikisha viongozi wa Serikali pamoja na kukemea maovu miongoni mwa
jamii bila woga.
W a n a n c h i w e n g i wamempongeza kwa uamuzi
aliochukua na kumtakia afya njema ili aweze kupona, kuendelea kutoa ushauri na
kuwataka viongozi wengine kuiga mfano wake.
Mtega
amelitumikia Jimbo la Iringa kwa miaka sita na baadaye Jimbo la Songea miaka 22
hivyo amekuwa askofu kwa muda wa miaka 28, Kiongozi wa Idara ya Elimu katika
Baraza Kuu la Maaskofu na Msimamizi wa kitume katika majimbo nane.
No comments:
Post a Comment