18 May 2013

Action Aid Tanzania kukabidhi mashine za kukamua alizeti leo


Na Mwandishi Wetu, Singida 
 SHIRIKA la Actionaid Tanzania litafanya uzinduzi rasmi na kukabidhi kwa vyama vya ushirika mashine ya kukamua mafuta ya alizeti kwa vyama vya Ushirika vya Mtinko na Ilongero.
Hafla hiyo itafanyika katika kata ya Mtinko iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini, ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii, Dkt. Lazaro. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana nkwa vyombo vya habari na Ofisa Uhusiano wa Actionaid Tanzania, Bw.Bright Warren alisema hafla hiyo itafanyika kuanzia asubuhi.
Alisema shirika hilo limeingia mkataba na benki ya CRDB kwa kuweka dhamana ya
fedha kiasi cha sh. milioni 100 ili vyama vya ushirika viweze kukopa fedha benki ili ziweze kununua mashine za kukamua alizeti kwa lengo la kuongeza thamani ya mazao na kuongeza kipato cha wakulima wadogo.
"Kwa utaratibu huu, kwa kuanzia mwaka jana 2012 mwishoni vyama viwili vya ushirika vya Ilongero na Mtinko vimekopeshwa kiasi cha sh. milioni 40,000,000 kila kimoja kwa ajili ya kununua mashine za kukamua alizeti na fedha za kununulia alizeti.
" Ta y a r i v y a m a h i v y o vimeshanunua mashine za kukamua alizeti na zinafanya kazi ya kukamua alizeti. Mkopo huo ni wa mzunguko ambapo vyama vya ushirika vinapaswa kurejesha mkopo wote katika kipindi cha muda wa miaka miwili na fedha zitakazorejeshwa zitakopeshwa jamii nyingine kupitia vyama vyao vya ushirika ama CBO za wanawake,"alisema Bw. Warren .
Alisema lengo la mradi huo ni kumwongezea mkulima uwezo wa kuongezea thamani zao la alizeti ili aweze kupata kipato zaidi kwa kuuza mafuta na mashudu badala ya kuuza alizeti ambayo haijaongezwa thamani.
"Hi i p i a n i k uwe z e s h a wakulima kuendeleza na kupanua miradi ya ufugaji kutokana na kujipatia mashudu ambayo ni malisho bora ya mifugo ya aina mbalimbali,"alisema.
Alisema shirika hilo linaamini kwamba mradi huo unatarajiwa kuwa chachu muhimu katika harakati za kupambana na umaskini na kuwaletea maisha bora wananchi.

No comments:

Post a Comment