18 May 2013

Mchakato kuunda mamlaka wanyamapori waanza


Na Grace Ndossa


 VIONGOZI wakuu wastaafu waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Wizara ya Maliasili na Utalii wamekutana pamoja katika kujadili namna ya kubadilisha idara ya wanyamapori na kuunda Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania
Akifungua mkutano huo Dar es Salaam jana Waziri wa Maliasili na utalii, Balozi Khamis Kagasheki amesema kuwa wameamua kuwa kutanisha Makatibu wakuu na Mawaziri pamoja na wakurugenzi wastaafu waliokuwa wafanyakazi katika wizara hiyo kujadili namna ya kuunda mamlamka hiyo.
Alisema kuwa katika mkutano huo umewakutanisha Mawaziri, Mkatibu wakuu, na wakurugenzi waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali katika wizara hiyo kutoa maoni yao na kwa namna
gani watabadilisha muundo wa idara ya maliasili kuwa mamlaka.
"Huu ni mkutano wa wadau wa maliasili na utalii pamoja na viongozi wastaafu waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali, kutoa maoni yao ni kwa namna gani ya kuunda mamlaka ya wanyamapori ambao ni kwa muda mrefu sasa tangu ilipotangazwa bungeni hawajakusanya maoni," alisema Bw. Kagasheki.
Alisema kuwa hii tunataka kubadilisha kutoka Idara za wanyamapori iwe mamlaka ya wanyamapori ambayo itakuwa huru katika kufanya maamuzi ya kulinda wanyamapori.
Hata hivyo, alisema kuwa kamati iliyoundwa ya kutembelea nchi nyingine kuangalia muundo wa kubadilisha idara hiyo kuwa mamlaka zinavyofanya kazi zake ambapo kamati hiyo ilitembelea Kenya, Botswana pamoja na nchi nyingine kuangali jinsi wanavyofanya kazi zao na kutoa maoni yao ni kwa namna gani wanaweza kulinda wanyama pori.
Balozi Kagasheki alisema kuwa hao ni viongozi tu bado mikutano ya wadau itakaa na kutoa maoni yao na mwisho watapata namna ya kubadilisha idara hiyo kuwa mamlaka na idara ya wanyamapori watabakia wafanyakazi wachache tu.

No comments:

Post a Comment