02 April 2013

Wawili wafariki dunia Dar


Na Leah Daudi

WATU wawili wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari lenye namba T 855 ATB aina ya Scania ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva ambaye bado hajafahamika akitokea Ubungo kuelekea Buguruni Jijini Dar es salaam.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Mkoa wa Kipolis Ilala, Marietha Minange alisema ajali hiyo ilitokea juzi 5:15 usiku katika barabara ya Mandela eneo la Tabata Relini.

Alisema gari hilo lilimshinda dereva huyo na kwenda kuangukia magari manne na pikipiki mbili ambazo  zilisomeka kwa namba T122 CDB bajaj Boxer na T 705 BSX Hiba ikiendeshwa na Hussei  Abdallah (43) mkazi wa Tabata akiwa amepakia abiria aitwaye Hashim Omary (21) mkazi wa Tabata.

Kamanda Minange alisema  dereva wa pikipiki namba T 705 BSX Hiba pamoja abiria wake walifariki dunia papo hapo.

Alisema kuwa katika ajali hiyo watu 7 walipata majeraha katika sehemu mbalimbali za miili yao na majeruhi 5 wamelazwa katika hospitali ya Amana.

Kamanda alisema kuwa majeruhi wengine wawili walitibiwa na kuruhusiwa,maiti zote zimehifadhiwa hospitalini hapo.

Wakati huohuo huko maeneo ya Magomeni Mikumi askari walifanya msako na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 21 wakiwa na bangi 147pamoja na pombe haramu ya gongo lita 30.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Charles Kenyela aliwataja watuhumuwa hao kuwa ni Hamisi Mashaka (25),Hamis Iddi(24),Azizi Katembo (27) Maneno Salum (26) Fatuma Yusuph (22) Philipo Mwakyoma (19) Omary Madoimla (22) na wenzao 14.




No comments:

Post a Comment