02 April 2013

Wanaigeria wakuhukumiwa miaka mitatu


Na Rehema Mohamed

RAIA watatu wa Nigeria wamehukumia kifungo cha miaka mitatu jera na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu au kulipa faini ya sh.100,000 baada ya kupatikana na hatia ya kuingia nchini bila kibali.

Raia hao ni Bw.Sikiru Ibrahim (47)mfanyabiashara aliyekuwa akiishi Palace Hotel Sinza tangu mwaka 2011,Bw.Ebrima Sallah (32) mcheza Mpira aliyekuwa akiishi Tabata tangu mwaka 2010 na Bw.Kayude Aina (54) mfanyabiashara aliyekuwa akiishi Sinza Mori tangu mwaka 2010.

Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki mahakamani hapo na hakimu Elimius Mchauru huku upande wa mashtaka ukiwakilishwa na wakili kutoka Idara ya UHamiaji Bw.Patrick Ngayomela.

Ilidaiwa kuwa Machi 22 mwaka huu eneo la Oysterbay Kinondoni,washtakiwa hao walikamatwa nchini bila ya kibari cha kuwaruhusu kuishi nchini.

Baada ya upelelezi wa tuhuma hizo kukamilika,na washtakiwa kuchukuliwa maelezo na ofisa wa uhamiaji Bw.Salum Nabaraka na Bw.Gwanafyo Mwakaunga ikagundulika kuwa  wamevunja sheria ya uhamiaji na ofisa wa uhamiaji wa mkoa akaamuru watu hao kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka.

Machi 27 mwaka huu washtakiwa hao waliletwa mahakamani kujibu mashtaka yao na kupatikana na hatia ambapo walihukukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani au kulipa faini ya sh.100,000 kila mmoja.Washtakiwa hao walishindwa kulipa faini hiyo na hivyo walipelekwa gerezani.



No comments:

Post a Comment