04 April 2013
Ujenzi wa vyoo shule ya Mengi waanza
Na Chrisina Mokimirya
UJENZI wa vyoo katika Shule ya Msingi Reginald Mengi, iliyopo Sinza, Dar es Salaam, umeaanza baada ya shule hiyo kukabiliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Mkuu wa shule hiyo, Juvenari Muta, alisema ujenzi huo upo katika hatua za awali ambao unafanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni.
“Vyoo vinavyojengwa ni zaidi ya sita ambavyo vitatumiwa na wanafunzi wote wanaume kwa wanawake...tumeambiwa idadi
ya vyoo inaweza kuzidi ile ya awali,” alisema.
Alisema kukamilika kwa ujenzi huo mapema, kutategemea na kasi ya wajenzi ili viweze kutumika kabla shule hazijafunguliwa.
Vyoo vya shule hiyo vilibomoka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
huku nako inabidi kuchunguzwe. kwanini kuwe na tatizo lavyoo kinondoni? wilaya hii ni tajiri lakini kuna mchwa anayetafuna mapato ya wilaya hiyo. kinondoni inatakiwa kuwa mfano kwa nchi nzima
ReplyDelete