04 April 2013

Lori lapinduka na kuua watatu Mto Wami


Na Masau Bwire, Bagamoyo

WATU watatu wamefariki dunia baada ya roli walilokuwa wakisafiria aina ya Nissan Dizel, lenye namba T 885 ACC,
kutoka Pangani, mkoani Tanga kwenda Dar es Salaam,
kupinduka na kutumbukia kwenye korongo lililopo
eneo la Mto Wami, Bagamoyo, mkoani Pwani.


Ajali hiyo imetokea juzi saa 12:30 asubuhi, baada ya breki za gari hilo, kushindwa kufanya kazi ambapo waliokufa ni dereba Iddi Abudul maalufu 'Zungu', utingo wake Emanuel Kimati na
mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Bakari ambaye
aliomba lifti akitokea mjini Korogwe.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema baada
ya breki za gari hilo kushindwa kufanya, lilibadili mwelekeo na dereva aliporajibu kurirudisha barabarani, liligonga kizuizi cha
bati pembeni mwa barabara na kujikita kwenye korongo refu.

Alisema watu wote watatu waliokuwemo katika gari hilo walikufa papo hapo na miili yao imeharibika vibaya ambapo mashuhuda wa ajali hiyo wakazi wa eneo la Wami, walisema, hawajawahi kushuhudia ajali mbaya kama hiyo katika eneo lao.

“Ajali hii ni mbaya, tangu niishi eneo hili sijawahi kuishuhudia,
gari lilipaa na kwenda kujikita bondeni kwenye korongo refu na watu wote walikufa kifo kibaya wakijiona,” alisema Bw. Juma Abraham.

Aliongeza kuwa, wakati lori hilo linapaa, utingo wake alichomoka kutoka kwenye gari na kurushwa bondeni ambapo lori hilo lilikwenda kumlalia.

“Ili kuitoa miili yao, tulilazimika kutumia shoka kuvunja mabati
ya gari, watu wote walikandamizwa na kichwa cha gari na miili
yao tulifanya kuikusanya vipande, vingine vikiwa vimetengana kabisa na viwiliwili vyao,” alisema Bw. Abraham.

Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya
ya Bagamoyo ikisubili kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari ili kukabidhiwa kwa ndugu zao.

1 comment:

  1. Siyo "roli" linaitwa LORI (neno hili linatokana na neno la kiingereza "lorry" - gari la kubebea mizigo. Wahariri, msichangie kuharibu kiingereza kwa kutohariri kwa umakini habari mletewazo na reporters wenu. Wengine hawajui Kiswahili


    ReplyDelete