02 April 2013

Taarifa ya CCM yamliza Mkapa


Cornel Anthony na Hamisi Nasiri, Masasi

RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa, juzi alishindwa kujizuia na kutoa machozi baada ya kupokea ripoti
ya uharibifu uliofanywe katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.

Uharibifu huo ulitokana na vurugu zilizochangiwa na taarifa
potofu juu ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka mkoani humo
hadi Dar es Salaam, Februari mwaka huu.

Katika ziara hiyo, Rais Mkapa alipata fursa ya nyumba za wabunge wa Masasi, Bi. Mariamu Kasembe na Bi. Anna Abdallah ambapo hivi sasa, chama hicho wilayani humo hakina ofisi wala vitendea kazi jambo linalokwamisha ufanisi wa shughuli za chama.

Akisoma taarifa hiyo, Katibu wa CCM wilayani humo, Bw. Cremensi Mponzi, alisema kutokana na uhalibifu huo viongozi
wa chama hicho wanapata wakati mgumu katika kutekeleza majukumu ya chama kwa kukosa ofisa ya kudumu.

“Katika vurugu hizi, thamani nyingi za ofisi zimeibwa zikiwemo kompyuta tano ambazo zilikuwa zikitunza kumbukumbu muhimu
za chama chetu,” alisema Bw. Mponzi.

Alisema pia chama hicho kimepoteza gari ambalo lilikuwa nguzo muhimu katika kufanikisha shughuli za chama ambapo hivi sasa, viongozi hulazimika kutembea kwa miguu ili kufanya kazi.

Aliongeza kuwa, baadhi ya shughuli za chama hushindwa kutekelezwa kwa wakati kutokana na ukosefu wa gari.

Kwa upande wake, Bw. Makapa baada ya kupokea taarifa hiyo, alichangia sh. 500,000 na kusema kuwa, taarifa hiyo imemsikitisha pamoja na kushuhudia mwenyewe uhalibifu wa mali za chama.

“Naomba niwape sh. 500,000 kama sehemu ya mchango wangu
kwa jinsi nilivyoguswa na maafa haya ambayo yamenisikitisha
sana nawapa pole nyingi,” alisema Bw. Mkapa.
                                       

41 comments:

  1. Usilie Mkapa, usilie. Kishauri chama chako na serikali wawe karibu zaidi na wananchi. Bomba si linajengwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. sawa kabisa,lakini anyamaze tu,hana sababu ya kulia,serikali yetu imedhani ni rahisi sana kututawala tukiwa wajinga na kwamba umaskini wetu ni mtaji wao wa kupatia fedha na kwa hiyo wameufanya kuwa endelevu, kwamba ni mradi wao na ujinga wetu ni wa kudumu,sasa wajue kwamba kutwawala maskini na wajinga ni bomu na linaweza kulipuka likaua wengi pamoja na waliolitega.

      Delete
  2. Unalia kwa Afisi tu imechomwa na itajengwa nyengine lakini Wa- Zanzibari wanalia mpaka leo kwa kuuliwa ndugu zao ambazo roho zao hazirudi tena na waliowauwa ni Serikali ya Chama chako cha CCM na wewe ukiwa Rais wa nchi

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe hata hujui unachosema. tazama mbele, acha uvivu wa fikra. acha uchochezi.

      Delete
    2. Bora umemwambia,yamkini hajui atendalo

      Delete
    3. Mungu ametupa akili , lakini tunatakiwa kufikiri kabla ya kusema .Tunatakiwa tujue hii ni Tanzania ya wote na raslimali ni za wote hata gesi na mafuta ni ya wote tuache ubinafsi, mbona mikoa mingine ilikuwa ikiitunza Mtwara miaka yote hailalamiki.Wanamtwara tuache siasa za uchochezi

      Delete
    4. wewe ndo hujui unachosema huwezi kusema Tanzania ni ya wote wakati unashuhudia raslimali za nchizinafaidiwa na wachache mafisadi wa ccm.Hata hivyo wanachodai watu wa Mtwara ni kiwanda cha kusindika gesi kijengwe huko kwao kama ilivyo kwa viwanda vya samaki vilijengwa kanda ya ziwa ,viwanda vya kusindika dhahabu viko huko huko kwenye migodi hata viwanda vya kahawa viko kilimanjaro na mbeya na hatukuwahi kusikia vinaenda kujengwa Mtwara au Lindi.Kwa hiyo watu wa ukanda huo nao wana haki ya kudai viwanda vya malighafi zinazopatikana maeneo yao vijengwe hukohuko.Tafakari kwa kichwa chako na wala usitumie kichwa cha watawala na wakoloni weusi.

      Delete
  3. mnafiki mkubwa huyo analia nini wakati yeye mwenyewe ndo aliendesha vita zaidi ya ubinadamu mkuda tu na si mali za chama hizo fala wewe ni mali za wananchi yeye kaua wangapiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
    Replies
    1. KWELI BENI KALILIA WAGONJWA WA AKILI SASA WANAMSHANGAA!!! MZEE UNALILIA WALEVI HAO. ONA WANVYOKUTUKANA. ULIKUA UKIHUBIRI BARABARA YA KIBITI LINDI, DARAJA LA MTO RUFIJI, MKURUBITA, MKUKUTA NA MENGI YA KUYAOKOA HAYO MAJINGA KUTOKA LINDI LA UMASIKIN. BADO WALIKUA WAMELALA SASA WAMESIKIA GESI AMABAYO HAWAWEZI KUIZALISHA ETI WAMEZINDIKIA KUKUTUKANA! TUNAKUPENDA, TUANAKUENZI ULISIMAMISHA HATA MFUMKO WA BEI NA FEDHA IKAWA NA THAMANI

      Delete
  4. Kinachomliza siyo kuchomwa kwa ofisi bali ni Hisia kali za unyumbani na hisia za utambuzi kuwa wanakusini wa leo wameerevuka hivyo wajanja kama yeye wako mashakani. KWANI ALIDHANI WATAKUBALI KUONEWA MPAKA LINI? KAKIMBIA KUWEKA MAKAZI HUKU KWAO ( KUSINI )ILI WAENDELEE KUHALALISHA UONEVU MAANA ANGELIKUWAPO HUKU WANGESITA KUFANYA MENGINE YA UONEVU KWA KUMUHOFIA MZEE MSTAAFU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. KWELI YUKO MASHAKANI KAMA ANGEKUA KATIKATI YENU. MLIVYOKOSA SHUKRANI TU. ETI SASA MMEKUA WAJANJA WA KUCHOMA NYUMBA ZA ZEWENU WALIOAJIRIWA NA CCM. MLIKUA MNATAKA WASIPATE MISHAHARA NINI? KWANI NINYI HAMJENGI AMA HAMNA MISHARA? AMA KAMA CCM NDIYO ILIYOKO MADARAKANI WATU WASIAJIRIWE? ACHENI UJANJA WA CHURA KUKIMBILIA MAJINI MVUA IKINYESHA!

      Delete
  5. Nawaomba wachapaji wa habari ktk gazeti hili muwe makini kwani yapo makosa mengi kiasi cha kupunguza utamu wakati wa usomaji.

    ReplyDelete
  6. Mkapa kama kweli umelizwa na ofisi kuchomwa basi nawe rudi nyumbani usaidie kuwaelimisha wenzio ustaarabu mbona umekimbilia Lushoto ni kwenu kule? au mmoja kati ya wazazi wako ana asili ya Tanga ndivyo Ngwilizi alivyokuambia?

    ReplyDelete
    Replies
    1. MZEE WA WATU ANGEJENGA HAPO SI MNGEMCHOMEA TU KAMA WENZAKE? HERI YEYE ALIKUA MJANJA AKAJENGA LUSHOTO. MLIVYOWASHIRIKINA NA ROHO MBAYA NANI AJENGE KWENU. WLIOJENGA SI MMEWACHOMEA NYUMBA ZAO ILI WOTE MBAKI NA MAKUTI MFANANE.

      Delete
    2. MKAPA ANALILIA OFISI!ROHO ZA WATU JE? MAESAHAU ALIVYOWAUA WAZANZIBAR.

      Delete
  7. kumbuka mgemuenzi Nyerere kwa vitendo yasingetokea hayo hata ukilia inaweza isisaidie kwa sababu unapolia wewe unafutwa machozi lkn kuna raia walibomolewa nyumba zao kwa ajili ya mradi huo hawana wa kuwafuta machozi

    ReplyDelete
  8. Serikali imezoeya kufanya kila kitu siri, na ndio maana watu wameibatiza kuwa ni SIRIKALI. Madhara ya sirikali... yaani kutowasiliana na wananchi hasa katika mambo nyeti yanayogusa maisha yao ndio vurugu kama hizo ambazo zinasababisha hasara za mali na maisha ya wananchi!

    ReplyDelete
  9. Hjalia kwa watu wa mtwara waliofariko na Skokie lwamba
    Watu wa mtwara hawajapewa maendele
    Miaka mends Rudi. Ms mkataba wa gesi bumu Kama kesi nyingi za tanesco.

    ReplyDelete
  10. hongera kwa kulilia kwenu kusini uzalendo huo ungeonesha na kipindi upo rais kusinge kuwa nyuma kimaendelea,maana hakuna usafiri wa ndege wa uhakika zaidi ya mtwara ndio kiwanja kinalami.lindi kiwanja kikubwa lakini hakuna lami wala ratiba ya ndege .wewe unalilia chama baada ya kulilia maendeleo kwenu kusini? tutawauliza viongozi wa kusini mukituka madarakani mmeonesha nini cha maendeleo mnatia aibu kabisa

    ReplyDelete
    Replies
    1. SIRI IMESHAFICHUKA. KUMBE MNACHOMA NYUMBA ZA WASOMI WENU WALIOAJIRIWA NA CCM. NDIO MAANA VIJI VINGI VIMEBAKI NYUMA HATA KAMA VINA WASOMI NA WATU WENYE KAZI NZURI. WIVU, USHIRIKINA, CHUKI, KWANINI KAPATA, KWANINI MTOTO WA FULANI.SASA NANI ATAJENGA TENA KAMA ANAJUA NYUMBA ITACHOMWA? MSIBABIDILIKA MTABAKI NYUMA MPAKA KIAMA. MMESIKIA NYUMBA ZA MAKADA WA CCM AKINA MENGI, AKINA MRAMBA, AKINA MSUYA ZIMECHOMWA? UPINZANI UKISHINDA OFISI ZA CCM SI ZITAKUA ZA UPINZANI? SI WANACHI WALIOZIJENGA? ACHENI ROHO MBAYA KAMA ZAO MNALOLIMA. MIRADI YA WALIOBAHATIKA HUA HUPAMBA NA KUINUA USTAWI WA MAHALI. VIJANA WANAPATA KITU CHA KUIGA.

      Delete
  11. WACHANGIAJI WENGI MNAONEKANA MNAROHO MBAYA? KAMA HUNA NENO NI BORA UKAE KIMYA,SIJUI UMASIKINI WA MAWAZO AU KIPATO NDIO CHANZO? MTAWACHUKIA WATU WOTE KWA SABABU YA UVIVU WENU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe unaonekana una four ya 31,na umevalishwa miwani ya mbao.

      Delete
  12. KWA KWELI NCHI HII KUNA UPENDELEO WA AJABU! NENDA K'NJARO UKAONE, BARABARA HADI VICHOCHORONI! HALI WANANCHI WA MIKOA MINGINE(HASA YA KUSINI) WAKIISHIA KUBUGIA VUMBI!!!! KWANI KULE K'NJARO NI KENYA AU NI TZ HII HII? SAFI SANA WANAMTWARA, MSIKUBALI UPUUZI WA NAMNA HII. BEN MWENYEWE KAENDA KUJENGA LUSHOTO, ETI HALI YA HEWA NZURI. MTWARA INGEKUWA HALI YA HEWA MABYA ANGEKUWA HADI KUWA RAIS?

    ReplyDelete
    Replies
    1. SIO HALI YA HEWA 'HEWA' NZURI. NI WATU WAZURI. WATU NDIO HALI YA HEWA. WEWE HUJUI MTWARA HALI YA HEWA MBAYA. MAANAKE WATU WABAYA!

      Delete
  13. WATU WA KUSINI TUMEJAALIWA KITU KIMOJA, ROHO MBAYA NA ZA KWANINI. HII NDIYO SABABU KUBWA AMBAYO IINASABABISHA MIKOA YA KUSINI INAKUWA MASKINI MIAKA NENDA RUDI.
    WATOTO WAKISOMA MNAWAONEA WIVU, AKIJA NA GARI MNAULIZA, HIVI MTOTO WA NANI HUYU, UKIAMBIWA WA MZEE KUNDAMBANDA BASI UNAANZA KUMROGA NA KUMPIGA MAJUNGU. SASA HAYA SIYO MAISHA. ETI UMEME UKIKATIKA KAMA WEWE HUNA UMEME UNASEMA KWA KUSHANGILIA,"AFADHARI UMEZIMIKA, TUFANANE".
    NGOJENI NIWAFUNDISHE KITU WANA KUSINI WENZANGU, HUKU KWETU HAKUKALIKI, UKIMWONA KAKAA BASI JUA NA YEYE KILA SIKU NGENDE NA SEHEMU NYINGINE KUJIGANGA ILI WACHAWI WASIMPATE.
    WAKIJA WATU WA KASKAZINI MNALALAMIKA WANAIBA, LA HASHA, WAO SI WEZI BALI WANAFANYA KAZI KWA AKILI NA MAARIFA NA KUJITUMA, NDO SABABU WANAFANIKIWA. SISI TUMEBAKI KUWATAZAMA, KUWASEMA, KUWASENGENYA NA KUWATUKANA, ETI WEZI, SI WEZI WALE, WANATUMIA AKILI.
    NA KAMA TUSIPOBADILISHA MISIMAMO TUTABAKI MASKINI MAISHA YETU YOTE MPAKA SIKU YA KIAMA.
    UKIMWONA MTU KAFANIKIWA, MUIGE ILI NA WEWE UFANIKIWE, SIYO KUMPIGA MAJUNGU WALA KUFIKILIA NAMNA YA KUMTOA UHAI WAKE.
    MSIWAONEE WIVU WENZETU WA KILIMANJARO, WAO WANATUMIA AKILI ZAO ZA KUZALIWA, SHULE WANAJENGA NA WATOTO WANAHIMIZWA NA WAZAZI WAO KUSOMA, SISI WAZAZI WETU WANATUHIMIZA TUKAZANE KUFANYA MAPENZI ILI WAPATE WAJUKUU, SASA WAJUKUU MWAWATAKA HUKU CHAKULA WALAU MLO MMOJA WAWASHINDA?
    VIJANA WA KIUME NA WA KIKE WANAFIKILIA MAPENZI TU, MPAKA VIJANA WA KIUME SIKU HIZI LINDI NA MTWARA WAMEKUWA MASHOGA,UNATEGEMEA NINI?
    AMKENI VIJANA, ACHENI KUWA NA MAMBO YA KIZAMANI KAMA WAZEE WETU, SISI NI DAMU CHANGA, TUJIKOMBOE NA SI KWA VITA, NI KWA KUSOMA, KUFANYA KAZI KWA BIDII NA MAARIFA.
    VINGINEVYO WATU WA KASKAZINI WATAKUWA WANAKUJA WANATUZALISHIA DADA ZETU, KISHA WANACHUKUA WATOTO ZAO WANAONDOKA.
    TUBADILIKE WAMWERA
    TUBADILIKE WAMAKONDE
    TUBADILIKO WAMAGINGO
    TUBADILIKE WAMATUMBI
    TUBADILIKE WA...........
    TUBADILIKE WANAKUSINI.
    KUSINI ITABADILIKA KAMA TUTABADILI FIKRA ZETU.

    ReplyDelete
  14. MZEE MKAPA TUTAKUENZI DAIMA. ULISIMAMIA MISINGI IMARA YA TAIFA LETU, HAUKUYUMBISHWA KWA FIKRA ZA KIBINAFSI, ULIKUWA MKWELI, ULIWEZA KUKEMEA MAOVU NA TAIFA LIKAPITA KATIKA KIPINDI KIGUMU KWA MAFANIKIO AMBAYO HAYAJAWEZA KUFIKIWA MPAKA SASA... "YOU ARE THE STONE THAT THE BUILDERS REFUSED..."

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe muongo embu tuambie maovu alio kemea,usidanganye watu bwana.

      Delete
  15. Mbona mnatuma maoni ya kashfa namna hii? Ninyi mliotuma maombi haya mnataka kusema mna haki mbele za Mungu kuwahukumu wengine? Acheni ujinga na uchochezi, tatizo hamtaki kutumia akili kujiletea maendeleo mnategemea serikali iwajengee nyumba, iwape kandambili hadi chumvi! Aah mnatia aibu. Maendeleo ya mtu ni mtu mwenyewe sio gesi wala serikali, ukishajengewa barabara ukawekewa umeme na maji, shule na hospitali unataka nini tena AU UWEKEWE NA VOCHA YA LUKU? Watanzania tusipende kugombana tubadilike mitazamo jamani lo!

    ReplyDelete
  16. Wakati mnajengewa barabara ya lami na lile daraja la mkapa mbona hamkuandamana kupinga pesa iliyozalishwa mikoa mingine isifanye kazi kwenu? Mtakosa fursa muhimu kwa sababu ya vurugu ambazo mngefuata utaratibu mambo yasingefika huko. Geita ni tajiri sana wa madini mbona wasiandamane kutaka pesa ya madini ibaki geita, WASUKUMA HOYEE! Ujinga ukichanganyika na umasikini huleta vurugu na maamuzi mabovu. Mnaacha kujenga nyumba za bati muingiziwe umeme kutwa barabarani kuandamana. Aliyesema maandamano huleta maendeleo nani. Pelekeni watoto shule, fanyeni kazi kwa bidii na heshimuni sheria bila shuruti au hadi Kenyela aje atangaze kuheshimu sheria. Pole sana rais Mkapa ila una kazi ya ziada ya kuwaelimisha wana mtwara wenzako labda utumie lugha ya asili huenda kiswahili kwao bado hakieleweki, maana mambo wanayofanya ni zaidi ya mtoto wa chekechea

    ReplyDelete
  17. mkapa hana jipya!

    ReplyDelete
  18. huyo mkapa aache unafiki mbona anashindwa kuwakemea hao mafisadi????????

    ReplyDelete
  19. Wewe una jipya? Umekririshwa chuki mpaka inakutia wazimu!!!

    ReplyDelete
  20. UMASIKINI MKUBWA WA WATANZANIA NI RASILIMALWATU NI VEMA KUJIULIZA KUWA NARASILIMALI ASILIA KAMA NI KIGEZO ZA UTAJIRI MBONA KONGO KINSHASA ZIKO NYINGI LAKINI NI YA KWANZA KWA UMASKINI TUJIULIZE NI KIGEZO KIPI KIMEFANYA JAPAN IWE NA MAENDELEO YA JUU LICHA YA UPUNGUFU WA RASILIMALI ASILIA WAO SIO MAZUZU

    ReplyDelete
  21. MKAPA NI MNAFIKI WATANZANIA WAKATI WA MABADILIKO NISASA

    ReplyDelete
  22. MMEANZA KUCHOMA MAJENGO...MMESHA JENGA UTAMADUNI....MWISHO MTACHOMANA WENYEWE...MAMBO HAYA HUWA HAYANA MWISHO....!

    ReplyDelete
  23. Kila mtu ajisemee mwenyewe, Mkapa ni Rais mstaafu sio vibaya akalia lakini ni mwenyeji wa kusini mwacheni aseme na wakwao ingawaje amechelewa kwenda huko. siku ileile alipaswa kwenda.
    naomba kujua je Baada ya kustaafu hakai huko kusini au anakaa wapi? hata majanga hayo hayajamkuta hayupo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani wewe unakaa wapi? Umesikia Mkapa anaishi nje ya nchi? Marais wote wastaafu wanaishi nchini. Kama walifanya makosa ni ya kibinadamu ndio maana hawajakimbia nchi. Siasa za sasa za chuki zitawakimbiza wazee wetu. Na watakaoingia madarakani watazichota ili kujihami watakapotoka madarakani watimue nje. Siasa hizi! Tutavuna tunachpanda

      Delete
  24. Amani iwe nanyi ..... kuna mambo mengi mngeweza kuzungumzia kuiweka nchi yetu ikae kwa amania lakini haya majungu kuhusu Mstaafu jamani jamani . tuijenge nchi yetu na siyo kuibomoa . tuongelee maendeleo na siyo mabaya yaliyotendwa. Tuna bahati sana watanzania lakini tukiendelea hivi tutaipoteza kabisa hii bahati na baraka tuliyokuwa nayo.
    ASanteni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wenzetu wameamua kuwekeza katika chuki na majungu kwavile kuna wajanja wamewaahidi mbingu. Utadhani wao ni miungu iliyotumwa ili kuigharikisha nchi kwa maouvu yake. Bahati mbaya wamezaliwa na kukulia humuhumu! Ni kizazi kilekile cha nyoka kinachosubiri nafasi kiteme sumu!

      Delete
  25. HAKUNA ALIYEONGEA CHA MAANA HAPO NI CHUKI TUPU WAPUUZI WOTE

    ReplyDelete
  26. HIHIHIHIHIHIHIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII AAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA MI NACHEKA TU, BAADA YA MATUSI NA LAWAMA WHAT NEXT.TUJIFUNZE KUCHAGUA NA KUWAJUA VIONGOZI WENYE KUTUFIKISHA MBALI SIO KWA MANENO YAO. PIA TUACHE USHIRIKINA KWANI BABU ZETU WALITURITHISHA MPAKA LEO UMASKINI UNAPAMBA MOTO TUGEUKIE UPANDE WA FIKRA TU.POLENI SANA KWA GHADHABU ILA HAINA MAJIBU MTAUWANA BURE.

    ReplyDelete