05 April 2013
...waapa kumtoa Lwakatare *Ni maamuzi ya Halmashauri Kuu, Lissu 'afunguka'
Na Goodluck Hongo
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeapa kuhakikisha Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Bw. Wilfred Lwakatare, ambaye anakabiliwa na kesi ya ugaidi,
anaachiwa huru wakidai kuwa, mashtaka dhidi yake hayana ukweli.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bw. Tundu Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Mbunge wa Singida Mashariki na mmoja wa mawakili wanaomtetea Bw. Lwakatare, alisema msimamo huo ni maamuzi ya Kamati Kuu ya chama hicho inayoendelea kikao chake.
Kikao hicho kinamalizika leo ambapo Bw. Lissu aliongeza kuwa, wajumbe wa mkutano wamekubaliana kupambana ili kuhakikisha Bw. Lwakatare anaachiwa huru.
Alisema chama hicho kinatengenezewa mazingiza ya kuonekana magaidi ambapo kwa mujibu wa nyaraka alizonazo, zinonesha Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Mwigulu Nchemba, alimtumia fedha sh. 50,000, Bw. Ludovick Joseph, ambaye ni mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo
Aliongeza kuwa, fedha hizo zilitumwa katika simu yake ya
mkononi na kusisitiza kuwa, kuna mambo yaliyojificha ambapo
wakati ukifika, kila kitu kitawekwa wazi.
“Bw. Nchemba alituma fedha hizi kupitia simu yake ya mkononi ambayo hata katika vitabu vya Bunge ipo Januari 14 mwaka huu,
saa tano asubuhi, tupo tayari kupambana na mtu yeyote ambaye atakuja mahakamani kutoa ushahidi dhidi ya Lwakatare,” alisema.
Alisema hivi sasa kesi hiyo imepangiwa Jaji baada ya yeye na mawakili wenzake kupeleka maombi Mahakama Kuu na itaanza kusikilizwa Aprili 15 mwaka huu.
“Mwanzo tuliambiwa CHADEMA ni chama cha Mtei na Mbowe, waksema cha watu wa Kaskazini, wachanga, Wakristo na sasa wanataka kukifananisha chama chetu na magaidi, haya yote
yatapita kwani Nelson Mandela wa Afrika Kusini aliwekwa
ndani lakini mwisho wa siku akawa rais,” alisema.
Akizungumzia madai ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Zitto Kabwe, kutaka kuuawa, Bw. Lissu alisema hizo ni mbinu zinazotumika kukichafua chama chao ambacho kinakubalika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MABADILIKO YA KATIBA NI MUHIMU TENA SANA WAKILI MARANDO NDIYE MWANASHERIA ASIYETUMIKA KUPINDISHA SHERIA NI VEMA UKIWA KIONGOZI WA CHAMA AU MWANACHAMA WA CHAMA FULANI KAMA VILE MTUHUMIWA ANAVYOMKATAA HAKIMU ASIYEKUWA NA IMANI NAYE AWE NA MAHAKAMA ISIRUHUSU MAWAKILI WATAKAOPINDISHA SHERIA IWAPO HUWEZI KUWA SHAHIDI WA MKEO ,MAMA YAKO BABA YA YAKO NA MWANAO CHADEMA NI CHAMA CHA MAJAMBAZINA MAGAIDI HAKINA TOFAUTI
ReplyDeleteMwenzetu umeshindwa kutoa hoja inayodhihirisha Chadema kuwa chama cha kigaidi na kijambazi huku ukijua fika chama cha kigaidi ni kipi kwa matukio ya kuteka,kutesa na kuua watu wasio na hatia na kuwabambikia kesi wasiohusika wanaeleweka watanzania wanajua chama hicho kinatumia mgongo wa dola kuhalalisha uchafu huo ndio maana wahusika hawachukuliwi hatua yoyote najua unafiki wenu unafikia mwisho muda mfupi ujao maana penye ukweli uongo hujitenga.
DeleteHata YESU alifanyiwa vile alivyofanyiwa pamoja na uungwana wake, watanzania tutaendelea kuwa wajinga na watwana wa waliomadarakani kwa woga wetu wa kuogopa mabadiliko. Asikudanganye mtu, hakuna maendeleo pasipo watu kujitoa muhanga, Chadema na wafuasi wake ndiyo waliojitoa kuleta mabadiliko lakini kwa ujinga na woga wa kijinga tunaponda juhudi hizi, sasa kwa nini mnalalamikia ugumu wa maisha? Amka watanzania, unga mkono Chadema
ReplyDeleteWEWE NA WENZAKO WENYE AKILI KAMA WEWE MNATOSHA KUSHIBIKIA CHADEMA, SISI HATUTAKI TUACHENI TUENDELEE NA CCM.
DeleteRWAKATARE NA YESU WAPI NA WAPI WALA YESU SI MUONGO ,WALA YESU SI MZUSHI ,WALA YESU N MZINIFU CHAMA CHA CHADEMA UADILIFU SIFURI WAO HATA SHETANI WANGEPENDEKEZA AINGIE MBINGUNI RASILIMALI WATU CHADEMA SIFURI KIMEJAZASATU WA KUPEPETA MIDOMO TU WALIPIMWA WAPI UTENDAJI NI SAWA NA KUOLEWA NA KICHAA UKIFIKIRI BAADA YA NDOA UPAKO ALIOUPATA BAADA YA NDOA UKICHAA UTAISHA
ReplyDeleteni chama gani cha wazinifu? umesahau wazinifu ni kina nani? katika historia nakumbuka wazinifu ni CCM kwani kipindi cha bunge miaka ya 90 hadi 2000 hii ilipitishwa tamko la wabunge kuandamana na wake zao kwenda dodoma baada ya uchangu doa kuzidi dodoma na hasa wakati wa bunge. mbona pia madai ya batilda kubeba mimba ya lowasa yeye batilda hakujitokeza kukataa madai hayo mahakamani? uzinzi gani wakati juzi tu arusha kafia guest kijana wa ccm kwa kuzidiwa majamboz na watoto wa arusha? uzinzi gani ambao inajulikana jinsi vyeo hasa kwa wanawake huko CCM vivyopatikana hasa unapokuwa karibu na wapambe wa mnene au ukaribu na mnene mwenyewe? uzinzi gani zaidi ya kuwapa ukuu wa wilaya kina fulani kwa kumridhisha ridhiwani ili amwombee ukuu kwa mnene?? acheni tunawajua vyema. kama mtaendeleza maneno ya kashfa bila kuzingatia sheria tutatoa laivu picha zenu ninyi wazinzi mastaa.
Deletekisaikolojia mtu husema kile kimkaacho moyoni ambayo ndio matendo yake ya kila siku. CCM ni wazinzi si uongo. tutawataja mastaa wanaongoza msipojirekebisha.
Maisha bora kwa kila mtoto wa kiongozi aliye serikalini
ReplyDeleteMTOTO WA RAIS HUWEZI UKAFANANA NAE WEWE KAPUKU? UBINAFSI HUO? KUWA WEWE BASI MTOTO WA RAIS.UVIVU UNAOKUSUMBUA HUO.
DeleteSasa kama unapigania kua kiongozi watoto wako watakua watoto wa nani kama sio wa kiongozi. Kwahiyo viongozi wasijali familia zao ili kukurisha wewe. Roho mbaya kama korosho. Kwani Uhuru Kenyata ni mtoto wa nani? Odinga mototo wa wani? Hata historia husomi. Hapo chuo unafanya nini?
Deletewe are tired of brutality of this gvt
ReplyDeleteFANYA KAZI KWA BIDII NDIO DAWA USICHUKIE WATU, UTAKUFA KWA PRESHA NA ROHO MBAYA YAKO, MAANA HUTAWAFIKIA HAO.
DeleteEti umechoka nanini? Brutality? Nenda Kenya, Uganda, Rwanda hata Marekani uvunje sheria uone. Hapa unakashfu raisi, waziri mkuu, mawaziri kweupeeeee hata hushughulikiwi. Nafikiri Ungeshukuru Mungu kutoa kashfa zako ukiwaTZ bila kutiwa kibano!
DeleteBoya hapo ananichefua anapopiga mbwambwa nadhani mifano ya ukichaa imemtawala wakati yeye ndo kichaa kabisa...unda hoja wewe acha kubwabwaja!
ReplyDeleteukweli, serikali, siasa, watanzania tuwe makini sana,swala la mambo ya ndan ya chama kuvuja ni uzembe wa hali ya juu hata kama inavosemekana CCM inahusika , haya mambo yote yanatuhusu katika chaguzi za 2015, MUNGU bariki Tanzania ....atuepushe na siasa chafu na watu wasiomuogopa pia ghasia zinazotaka chafua akili za watu
ReplyDeleteCCM acheni uhuni kutumia mbinu mbaya kuchafua vyama vingine itawagarimu
ReplyDeleteWatanzania wanapaswa kufikiri kwa kutumia akili na busara ambazo hawakupewa na chama chochote, bali tangu walipozaliwa. Watanzania wengi wanapelekwa kama boya bila kujua wanaishia wapi kwa kuwa ni wavivu wa kutumia akili na BUSARA waliopewa na MUNGU, badala yake wanategemea akili na busara za watu wengine ambao baadhi yao au wengi wao hawana nia njema nao.
ReplyDeleteZile enzi za ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI zimepitwa! pengine zilikuwa sahihi wakati huo, lakini sii wakati huu wa sayansi na TEKE LINALOKUJA na DIGITAL ... au kwa kifupi .. UTANDAWAZI! Watu wawe wabunifu wawe na uwezo wa kuwawajibisha viongozi kuanzia ngazi ya familia hadi ya kitaifa, watafute habari za kitaifa na kimataifa. Kwa kupata habari hizi watu watapanuka AKILI watakuwa na uwezo wa kuchambua UKWELI na UONGO; watajua haki zao za msingi; watakuwa majasiri wa kuhoji viongozi kuhusiana na haki hizo; watakuwa na uwezo wa kuamua ni viongozi gani wanawataka.
Inasikitisha kuona watu wanaonekana waerevu na wasomi wanatetea viongozi au kundi ambalo linaonekana kushindwa kutekeleza wajibu wake hata na watoto wadogo. Kuwa na elimu kubwa ya darasani haimaanishi kuelimika.... wakati mwingine badala ya elimu ya darasani kupunguza ujinga kwa wengine inaongeza ujinga. AMKA MTAZANIA, ACHA KULALA!!
Mzalendo na mwelimishaji wa jamii
Tanzania.
WALIPOKUWA WANAULIWA CUF NA KUWEKWA NDANI NYINYI MLISEMA CUF WAONGO,WOGA NAWAZUSHI .SAA VIPI NA NYINYI HUKO TUSEME NINI?
ReplyDeleteCCM mna uhakika mbinu hizi zitawavusha 2015.Bado parefu sana na mnaonekana kuishiwa ile sifa yenu ya uintelijensia, mnajua kwa nini? mmeziba macho na masikio, mnaona visiyoonekana na kusikia visinyosikika, madaraka yamewalevya kama mlevi wa pombe..Sisi si wasomaji wazuri wa vitabu. Tafuteni kitabu kiitwacho SHAMBA LA WANYAMA (ANIMAL FARM)cha GEORGE ORWELL. Angalia wanyama walioonekana werevu na wenye uchungu na shamba lao/nci (NGURUWE)walivyowageuka wenzao baada ya kushika madaraka ya shamba (nchi) hilo baada ya kumuondoa mmiliki kwa mapinduzi. Nguruwe hao ndo CCM hapa kwetu. someni kitabu hicho.Mwisho wa nguruwe wale ndo utakuwa mwisho wa CCM
ReplyDeleteNYINYI CHADEMA MNAFANYA UHUNI NA UJAMBAZI MKIKAMATWA MNASINGIZIA CCM,SOMENI HISTORIA YA CCM VIZURI NDIPO MTAKUA NA HAKI YA KUKITUHUMU CCM.ACHENI KUKURUPUKA NYIE, NJAA HIYO NDIYO INAYOWASUMBUA, MKO TAYARI WATANZANIA WAUANE ILI MINGIE IKULU, HAMTAFAULU NG'O, POLENI SANA NA CHUKI ZENU HIZO
Deletemambo wanayofanya CCM wanadhani watanzania ni walewale wa miaka yote wanaowatumia na kuwabadilisha vichwa vyao wanavyotaka!!! mmechelewa ukweli tumewakataa hata mfanye hila gani TIME IS TELLING muondoke tumewachoka aaaaaaaaaaah......
ReplyDeleteNyie si wasomi msio na ajira. Woga wa maisha. Jengenei hoja za maendeleo. Watanzania wangefikiriaje wakati walikua hawawezi kusoma na kundika? Sasa wamepelekwa shule wanaweza kujitambua vizuri zaidi. Subiri ballot box. Mcharuko mtandaoni ni watu wachache sana ukilinganisha na watu zaidi ya million arobaini tano. Siasa sio mtaji na haibadili lolote. Watumishi wa ummma watabaki walele miaka yote. Watanzania watabaki vilevile kama Kenya, Malawi, zambia etc. Wanasiasa wataendelea kutafutana, kulipiziana visasi, na maisha ya watu wa kawaida yataendelea kama kawa. Just a change in figurehead.labda ujenge Chavez ama Kim mwingine ambaye hategemea mabepari wa nje
Deletekama kuna chama kinawaongoza watanzania kikiwa nje ya maeneo watanzania walipo ni CCM. wanawasahaulisha watanzania maumivu wanayoyapata kwa kuibua madai ya kitoto, matusi, kejeli, na vijembe.
ReplyDeleteHONGERENI SAAAAANA WANA-ccm.
ccm - CHAMA CHA MAAFA, CHAMA CHA MATUSI, CHAMA CHA MASINZI, CHAMA CHA MATUMBO, CHAMA CHA MAFISADI, CHAMA CHA MAJINGA, CHAMA CHA MAGAIDI, CHAMA CHA MASHETANI, CHAMA CHA MAKEJELI. yaani ccm acha tu jamani.
Aliyekupandikizia hii chucki umuombe pia akuajiri ukimaliza chuo. Amefanikiwa kwa asilimia mia. Sasa ni jukumu lake kukulipa ujira. Asipokulipa mgeuzie kibao
DeleteWAFUASI WA CHADEMA MNACHUKI, POLENI SANA, SIJUI MNASUKUMWA NA UCHU WA MADARAKA? HAMPATI NG'O MADARAKA, MTAISHIA MAJIMBO YA WAHUNI TU.
ReplyDeleteCHADEMA NI MCHARUKO TUPU. KILE MWENYE HEKIMA ANAYEJARIBU KUWAELEZA WATAMJIBU KWA JAZIBA. ONA WALIVYAHARIBU BUNGE, ONA WANAVYHARIBU VYUO NA WANAFUNZI MASHULENI. MCHARUKO TUPU KILA MAHALI. TUKIWAPA MADARAKA WATAJADILIANAJE? WAJUE WAKIWA MADARAKANI NDIO WATAWAJIBIKA KWA KILA JAMBO. SASA KAMA NI KASHFA KILA MAHALI WATAWEZA KUTULIZA AKILI ZAO AMA ITAKUA NI MUENDELEZO WA KUTOKUA WASIKIVU? HAO WENZANGU HATA PROFESA KAMA LIPUMBA AKIWASHAURI WATAMCHARUKIA TU.
DeleteSIWASHAURI WATZ WENZANGU KUIUNGA MKONO CHADEMA JAPO MIMI SI CCM. JAMANI UONGOZI ACHA WATU WAKUPE WENYEWE KWA KUZIONA JITIHADA ZAKO NA HEKIMA ZAKO UONGOZI HAUOMBWI WALA HAUDAIWI. MABADILIKO NI JAMBO ZURI LAKINI KAMA HUNA KILICHO BORA ZAIDI KILE ULICHONACHO NI BORA UKAWA MPOLE. MFANO WAKE NI KAMA KUPIGA DEKI KWA MKOJO KWA KUWA ETI UMEKOSA MAJI HAPO UTAKUA UNACHAFUA ZAIDI. CHADEMA NI KIZAZI CHA BONGO FLEVA NA MASHARO BARO, NI WASOMI WASIO NA HEKIMA. ELIMU NI UGALI MBOGA YAKE NI HEKIMA. KATU HAMTAPIGA HATUA NDUGU ZANGU MAANA KWAO WAO WANACHAGUA NEMBO YA CHAMA NA SI WATU TAHAMAKI NCHI ITATAWALIWA NA WASANII KAMA DAIMOND, MR BLU CHEGE NA TMK MAJITA UTAWAKUTA BUNGENI HALAFU SPIKA ATAKUA CHIDI BENZINO YANI TUTASHUHUDIA NGUMI TU BUNGENI. MKIBISHA FANYENI HALAFU NITAWAKUMBUSHA HAYA NILIYOYAANDIKA LEO. KENYA WALIHANGAIKA MATOKEO YAKE WAMERUDI PALE PALE JE NA WALE WALIOKUFA, HAWAKUJUA MASIKINI MUNGU AWAREHEMU WOOOTE AAMIN.
ReplyDeleteccn imechoka wanachojua ni kuburuza na taswira ya usanii uliotukuka na si vinginevyo.
ReplyDeleteNdipo upeo wako wa kufikiri ulikofikia. Unaburuzwa kwani huna akili! Wenzako wamejenga shule, vyuo vikuu, mabarabara, hduma ya mama na mtoto na kuweka uhuri wa kisiasa na ndio unaoutumia sasa kujieleza. Jitahidi pia kujikomboa kiuchumi. Fanya kazi kwa bidii, tafuta ajira inayolipa vizuri, ungana na vikundi vya ujasiriamali gombea hata ubunge ukiweza!Tumia fursa zote zilizopo utafanikiwa! Wote tumetoka vijijini.
DeleteKweli tumetoka kijijini, tuko mjini kutafuta! Kama chadema inakupa fursa, safi sana. Kama ni ccm basi tena. Nane ambaye ana ajira akakataa mshahara? Hao malaika wanaotokea kwenye baa alafu wanatutangazia mbingu labda ni malaika wa shetani.
Delete