02 April 2013

Mwanamke abakwa na kisha kunyongwa

Na  Prosper Mgimwa

Sumbawanga

MWANAMKE  mmoja  amefariki dunia baada  ya kubakwa na kunyongwa kisha mwili wake kuutelekeza njiani katika kijiji cha Kipabonde Ziwa Rukwa Wilayani
Sumbawanga mkoani Rukwa.


Tukio hilo lilitokea usiku wa Machi 24 mwaka huu,  ambapo Kamanda wa polisi Jacob Mwaruanda alisema watu waliofanya tukio hilo walimbaka kwanza kisha kumnyonga shingo .

Mwaruanda alisema kuwa bado Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na pindi utakapokamilika  na kuwakamata watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili za mauaji.

Na katika tukio jingine watoto wawili wamenusurika kifo baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kushika moto ulioshababishwa na kibatari katika kijiji
cha Singiwe kata  ya Matai Wilayani  kalambo Mkoani Rukwa.Kamanda  wa polisi Mkoani Rukwa  Jacob Mwaruanda  alisema kuwa watoto hao
walijeruhiwa  sehemu mbalimbali za miili yao na kufikishwa kwenye kituo cha
afya kwa matibabu.Aliwataja watoto hao kuwa ni Gabinus Nkanga(12) na Maria Nkanga(8) wote ni
familia moja ambapo hasara iliyopatikana   ni zaidi ya  milioni tano
inadaiwa  kuwa nyumba hiyo ilikuwa na chumba cha duka.Hata hivyo  kamanda wa polisi mkoani Rukwa  amewataka wananchi kuwa
makini  nyakati
za usiki  na vibatari hasa kwa watoto ili kuondokana na suala la janga moto.

No comments:

Post a Comment