02 April 2013

Adaiwa kumbaka mjukuu wake hadi kumpa ujauzitoNa Abdallah Amiri,
Nzega

JESHI la Polisi wilayani Nzega mkoani Tabora Linamshikilia mkazi mmoja wa kijiji cha Mwamala
Haji Onjaonja (65) kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake
hadi kumsababishia ujauzito.


Mkuu wa polisi
wilaya ya Nzega Yusuph Sarungi amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza
kuwa tukio hilo limetokea baada ya mtoto huyo kuonesha dalili za ujauzito.


Sarungi alisema
kuwa mtoto huyo akisoma kidato cha kwanza shule ya sekondari mwamala iliyopo
katika kata hiyo.

Mtoto huyo ambaye
jina lake anaitwa Tatu Nicholous (16) alikiri kufanyiwa kitendo hicho na
mtuhumiwa Haji Twalibu ambaye ni Babu yake wakati mkewake akiwa safarini Dar es
salaam.

Taarifa kutoka
katika zahanati ya mwamala zimethibitisha kuwa mtoto huyo anaujauzito wa miezi
mitano ambapo dalili zilianza kuonekana akiwa shuleni hapo.

Diwani wa Kata hiyo
Hamis Shomali amewataka wanafunzi wazingatie masomo pomoja na kutoa taarifa
mapema kwa wazazi endapo wapatapo matatizo wakiwa shuleni.

Shomali aliwataka
wananchi kulinda watoto hao wa shule ili kukuza elimu na kuongeza kuwa watu
watakaobainika kuwalaghai wanafunzi hao watachukuliwa hatua kali za kisheria
ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.

Sarungu amesema
kuwa upelelezi utakapo kamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu
tuhuma hizo zinazo mkabili.


No comments:

Post a Comment