02 April 2013

Madeva 5000 ukosa ajira kila mwaka kwa ukosefu wa viwangoNa Veronica Ikonga

MUUNGANO wa madereva wa malori na mabasi Tanzania (TDACCT) wamesema zaidi ya madeva 5000 wanakosa ajira kutokana na kukosa viwango vinavyostahili.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Muungano huo, Juma Machefu kwa Waandishi wa Habari alisema moja ya kanuni wanazozifuata ni kuangalia kuwa dereva ana uzoefu na kazi hiyo, hivyo anayebainika ndiye hutumikia chombo husika.

Alisema kuwa kuna changamoto nyingi zinazowakumba madereva ikiwemo ya madereva kutokuwa na leseni na bima ya maisha,hivyo huchangia anapopata ajali kupelekwa mahakamani huku mwenye gari akipata gari mpya,"alisema.

Machefu alisema kuwa katika muungano huo watahakisha kila dereva anakuwa na mkataba wa kudumu ili kuondoa usumbufu kwa muhusika na familia zao.

Aliipongeza Wizara ya kazi kwa kuonesha ushirikiano mzuri wa kuwaunganisha katika sekta hiyo licha ya SUMATRA kuwa chanzo cha kuwagonganisha madereva na Serikali kwa kukaa kuwaunganisha na wizara ya kazi.

Kupitia ushirikiano wa wizara ya kazi serikali imejua umuhimu wetu hivyo kuunda bodi ya usafirishaji ambayo inasaidia kutatua matatozi yanayojitokeza ikiwa ni moja ya kutafuta haki zetu,"alisema

No comments:

Post a Comment