02 April 2013

Kesi inayomkabili Mhasibu TRA kusikilizwa Aprili 2 mwaka huu


Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 2 mwaka huu inatarajiwa kuanza kusikiliza utetezi wa kesi ya kutakatisha fedha inayomkabli aliyekuwa mhasimbu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Bw.Justice Katiti.


Mbali na Bw.Katiti,washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mkurugenzi Mtendaji wa East Africa Procurement Service Ltd Bw.Gidion Ottulo, Mkurugenzi Mtendaji wa Romos Technology Ltd Bw.Robert Mbetwa na Bi.Lulu Chiza mfanyakazi wa Benki ya Barclays.

Washtakiwa hao wanatakiwa kujitetea baada ya mahakama hiyo kutoa uwamuzi kuwa wana kesi ya kujibu uwamuzi ambao ulitolewa mahakamani hapo juzi na Hakimu Bi.Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo.

Katika kesi hiyo washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Julai ,2008 Dar es Salaam walitenda kosa la kuhamisha sh.milioni 262,434,570 kutoka TRA .

Ilidaiwa kuwa Julai ,2008 Dar es Salaam Bi.Chiza akiwa mfanyakazi wa Barclays alihamisha fedha hizo ambazo zilitakiwa kulipwa kama kodi ya mapato kwa TRA.

Kwa upande wa mshtakiwa Bw.Katiti anadaiwa kuwa Agosti ,29,2008 Ilala Dar es Salaam akiwa kama mhasibu wa TRA kwa nia ya kumdanganya mwajiri wake aliandaa hati ya malipo ya kodi akionesha kuwa kampuni ya Sachak Plastics LTD ililipa kiasi hicho cha fedha.

Shtaka lingine ni kwamba mshtakiwa Bw.Ottulo,Bw.Mbetwa na Bi.Chiza wanadaiwa kumsaidia Bw.Katiti kutenda kosa la kujipatia sh.milioni 262 kwa malengo ambayo hayakukusudiwa.



No comments:

Post a Comment