02 April 2013

Kikwete aongoza waombolzaji kumuaga Mbunge

Na Goodluck Hongo

RAIS Jakaya Kikwete jana aliwaongoza viongozi mbalimbali wa Serikali na Wabunge katika kuuwaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Chambani Pemba visiwani Zanzibar aliyefariki juzi katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Rais Kikwete aliwasili majira ya saa tatu asubuhi akiwa na mkewe mama Salma Kikwete katika ukumbi wa karimjee jijini Dar es Salaam ambapo mwili wa mbunge huyo uliwekwa kwa ajili ya watu kuuaga kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar kwa mazishi.

Viongozi hao akiwemo makamu wa Rais Dkt.Mohamed Ghalib Bilali,Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiwemo na viongozi kutoka vyama vya mbalimbali vya siasa ambao walifika kutoa heshima zao za mwisho kwa mbunge huyo.

Akisoma wasifu wa marehemu wakati wa  kuagwa kwa mwili huo kaimu katibu wa bunge Bw.John Joel alisema marehemu Salimu Hemed Khamis alizaliwa shehia ya mizingani septemba 20,1951 jimbola Chambani Visiwani Zanzibar ambapo mwaka 1959-1960 alisoma katika shule ya msingi Pandani.

Alisema mwaka 1960-1967 alihamia na kumalizia shule ya msingi Kengeja ambapo mwaka 1968 alijiunga katika shule ya sekondari Chambani iliyoko Chambani Pemba hadi mwaka 1969.

"mwaka 1970 marehemu aliendelea na masomo ya sekondari katika shule ya Fidel Castro na alihitimu mwaka 1971 ambapo kwama 1972 alijiunga na shule ya sekondari Lumumba zamani ikiitwa Lumumba College kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na sita na kuhitimu mwaka 1973"alisema Bw.Joel.

Kwa upande wake Spika wa Bunge Bi. Anne Makinda alisema marehemu alikuwa mcheshi wakati wote hata alipotoa hoja zake bungeni hakuwa na kinyongo awapo nje ya bunge tofauti na wabunge wengine.

"Marehemu hiki kilikuwa kipindi chake cha pili bungeni kwani hakuwa na kinyongo na mtu hasa wakati wa kutoa hoja zake na hata alipotoka nje ya bunge aliendela kuwa mcheshi tofauti na wabunge wengine."alisema Bi Makinda

Naye katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dkt.Wilbroad Slaa alisema amefahamu marehemu tangu akiwa bungeni mwaka 2005 hadi 2010 na kwamba marehemu Salimu alikuwa makini sana katika kazi zake kwani alikuwa Waziri kivuli wa kilimo ushirika na chakula na yeye akiwa kama naibu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.

Kwa upande wake naibu katiku Mkuu bara wa Chama cha wananchi (Cuf) Julias Mtatiro aliwataka wananchi wa Pemba  kuwa watulivu wakati huu ingawa wamepoteza kiongozi mahiri kwa chama chao kwani alikuwa mtu wakutatua migogoro iliyokuwa ndani ya chama hicho.

Marehemu Salimu Hemed Khamisi ameshika nafasi mbalimbali katika uongozi wa chama cha CUF ikiwemo mjumbe wa kamati ya utendaji jimbo la Chambani na mjumbe wa kamati ya utendaji ya wilaya ya Mkoani Pemba tangu mwaka 2005 ambapo hadi anafariki alikuwa mbunge wa Chambani kwa tiketi ya Cuf.

Marehemu Salimu ameaacha vizuka viwili (wake) na watoto nane ambapo kabla ya umauti kumkuta aliangika ghafla katika ofisi ndogo za bunge baada ya kupata shambulio la kiharusi ambapo alifariki dunia juzi.

No comments:

Post a Comment