02 April 2013

Simba, Toto Africans hakuna mbabe



Na Daud Magesa, Mwanza

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacm Simba, jana walitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Toto Africans katika mechi ya ligi hiyo iliyochezwa Uwanjwa CCM Kirumba jijini hapa

Matokeo hayo yameifanya Simba kufikisha pointi 35 na kuendelea kung'ang'ania katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo.

Simba iliunza mpira kwa kasi ambapo ilishambulia lango la Toto, kama nyuki lakini washambuliaji wake Ramadhan Singano 'Messi' na Abdallah Seseme ambao walikosa mabao mengi ya wazi.

Hata hivyo ulibadilika na Toto kulishambulia lango la Simba, ambapo dakika ya 24 ilipata bao kupitia kwa Mussa Saida kwa shuti kali, baada ya kupokea pasi ya James Magafu.

Lakini bao hilo lilidumu kwa dakika mbili ambapo, Simba ilisawazisha kupitia kwa Rashid Mkopi.

Katika kipindi hicho Simba iliwatoa Jonas Mkude na Mkopi nafasi zao zikachukuliwa na Mrisho Ngasa na Ramadhan Kipalemoto.

Toto nayo ilimtoa Herry Mohamed na kumwingiza Selema Kibuta.

Mabadiliko hayo yaliongeza kasi kwa Simba na kufanya mashambulizi langoni mwa Toto, ambapo Ngasa alikosa bao baada kushindwa kuunasa mpira uliopita mbele yake.

Dakika ya 62, Ngasa alisawazisha makosa yake baada ya kuipatia Simba bao la pili kwa shuti kali akiwa umbali mita 35 baada ya kupokea pasi ya Haruna Chanongo.

Hata hivyo Toto ilisawazisha bao hilo dakika ya muda mchache baada ya kufungwa kupitia kwa Mohamed Netto, akipokea pasi ya Emmanuel Swita.

Hadi mwamuzi wa mechi hiyo anamaliza mpira timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2.

No comments:

Post a Comment