02 April 2013

Kaya 4,092 kujengewa vyoo vya kisasa


Na Mercy James,Njombe

HALMASHAURI ya Wilaya ya Njombe inatarajia kuendesha mpango wa kujenga vyoo bora
katika kaya zaidi ya 4,092 kwa kipindi cha miaka minne ikiwa ni kampeni ya kitaifa
ya kuzifikia kaya 100,000 ifikapo mw2aka 2015.

Kampeni hiyo imeanza kutekelezwa wilayahi humo kwa kuanza na kata 14 katika kata tatu na ufadhili wa shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF likifadhili mradi huo katika vijiji 18 katika kata tatu pia.

Akizungumza katika warsha ya siku moja ya Kamati za maendeleo ya kata (KAMAKA) kwa madiwani wa kata 28 wa wilaya hiyo, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bw. Conrad Ugonile alisema, mpango huo umekuja baada ya serikali kuzindua ya kampeni ya kitaifa ya usafi wa maingira kuanzia mwaka 2011 na kukamilka 2015.

Dkt. Ugonile alisema, katika wilaya ya Njombe, serikali inatarajia kutekeleza mradi kipaumbele kikiwa ni kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inakuwepo katika maeneo ambayo mradi huo utaanza kutekelezwa.

Alisema, kukosekana kwa vyoo bora, wananchi wamejikuta wakipata maambukizi ya vimelea vya magonjwa ya kuhara , damu na homa za matumbo,si kukosekana kwa vyoo tu pia huduma ya maji safi na salama inachangia kuwepo kwa magonjwa hayo kwa asilimia 35 hadi 37.

Utafiti wa wataalamu wa afya pia wamebaini kuwa tabia ya kunawa mikono,kwa sabuni inapunguza kwa asilimia 50 ya kuumwa magonjwa ya kuhara na matumizi ya vyoo bora yanapunguza hatari hiyo kwa asilimia 32.

Akitoa elimu kwa madiwani hao, afisa afya wilaya hiyo Remijus  Sungu alisema,idadi ya vitongoji 75 vinatarajiwa kufikiwa na mradi huo kwa mwaka wa kwanza na kuboresha vyoo 90, wakati watoa  huduma ya usafi wa mazingira watakuwa 17 kiwilaya.

Alisema, kampeni hiyo haitaishia katika kaya
pekee pia shule za msingi na sekondari 812 zitajengewa vyoo bora, na huduma ya maji
safi na salama ili kutekeleza kampeni ya kunawa mikono kwa maji safi baada ya kutoka kujisaidia, ambapo uvunaji wa maji ya mvua na uchimbaji wa visima utafanyika katika vijiji ambavyo vina tatizo hilo ili kufikia malengo.

Upande wao madiwani hao,Andrew Mangula diwani wa kata ya Saja, alishauri kuwa elimu
itolewe kwa jamii kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa kutunza mazingira, hususani
ujenzi wa vyoo ili kuepukana na tabia iliyojengeka katika jamii kujenga nyumba nzuri
na kushindwa kujenga vyoo bora.

Mangula alisema, pia kuna umuhimu wa kuwepo wataalamu wa kuhamasisha kila kata
kuwepo mtaalamu mmoja ili elimu hiyo iwe endelevu ili kuepusha watu kuendelea kula kinyesi katika uhalisia ili utekelezaji uendane na elimu.


No comments:

Post a Comment