02 April 2013

Akutwa chooni akiwa amejinyongaLeah Daudi na Neema Malley

MWANAUME mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Baraka Iddi anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (25-30) mkazi wa Mbweni amekutwa chooni amejinyonga kwa kutumia kamba.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Charles Kenyela alisema tukio hilo lilitokea juzi 2:30 asubuhi katika maeneo ya Mbweni Jijini Dar es salaam.

Alisema marehemu alikuwa mfanyakazi katika sehemu ya ujenzi ya Inocent Ngalunda (55) Mkuu wa chuo cha Takwimu mkazi wa Mbweni.

Kamanda Kenyela alisema sababu za kujinyonga bado hazijafahamika kwani marehemu hajaacha ujumbe wowote,mahiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala,upelelezi unaendelea.

Katika tukio lingine huko maeneo ya Mburahati Mabibo askari walifanya msako na kufanikiwa kuwakamata watuhuumiwa 10 wakiwa na bangi puli 10 kete 30 pamoja na pombe haramu ya gongo lita 25.

Kamanda Kenela aliwataja watuhumiwa hao kuwani Marehemu Matumbwa(27) Ramadhani Yahaya (19) Ibrahimu Mussa (39) Bakari Shabani (26) na wenzao 6.No comments:

Post a Comment