05 April 2013

Askofu Lukosi mbaroni, akutwa K'njaro akihubiri


Na Florah Temba, Moshi

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro, limemkamata Askofgu Romanus Lukosi wa Kanisa la Evangelist Assemblies Of God, lililiko Makambako, mkoani Njombe ambaye aliondoka nyumbani kwake Machi 22 mwaka huu, katika mazingira ya kutatanisha.


Askofu huyo ambaye inadaiwa alitekwa, jana alikutwa katika nyumba ya kulala iliyopo Majengo, Manispaa ya Moshi Mjini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kkamanda wa Polisi
mkoani humo, Bw. Robert Boaz, alisema askofu huyo aliondoka nyumbani kwake bila ya kutoa taarifa hivyo kuzua hofu katika familia na kanisa lake.

Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, askofu huyo amekutwa akiwa anafanya maombi katika eneo hilo ambapo kutoweka kwake nyumbani bila kuaga kulisababisha vyombo mbalimbali
vya habari kuripoti kuwa ametekwa.

“Askofu Lukos aliondoka nyumbani kwake bila kutoa taarifa
za mahali aliko kwa kipindi cha wiki mbili hivyo kusababisha vyombo mbalimbali vya habari kutangaza ametekwa na watu wasiojulikana na kusababisha hofu,” alisema.

Alisema jeshi hilo limemkamata jana asubuhi eneo la Majengo akifanya maombi na kutumia fursa hiyo kuitaka jamii ijenge
tabia ya kuchunguza taarifa wanazozipata kabla ya
kuzisambaza ili kuondoa hofu.

Aliongeza kuwa, uchunguzi wa awali umebaini askofu huyo baada ya kuondoka nyumbani, alienda mkoani Morogoro, Pwani, Dar es Salaam na hatimaye Kilimanjaro alikokamatiwa na hivi sasa wanaendelea kumuhoji.

Akizungumza na waandishi wa habari, askofu huyo alisema hakuwahi kutekwa kama ilivyodaiwa na vyombo mbalimbali vya habari bali aliamua kuondoka kwenda kutafuta eneo tulivu la kufanyia maombi kwa siku saba bila usumbufu.

Alisema kutokana na hofu iliyojengeka katika familia yake na
kanisa, imekuwa fundisho kwake na hataweza kuondoka tena
bila ya kuaga na kutoa taarifa.

14 comments:

  1. Wahubiri wengi wa siku hizi ni wajasiriamali tu hutumia dini kujitafutia riziki tofauti na mafundisho ya bw.Yesu kristo aliyeutafuta ufalme wa mbinguni bila kuendekeza mali na utajiri.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi kweli kuna sehemu yenye vurugu nyingu hapa Tanzania kuliko Dar?
      Inakuwaje Mchungaji adai alikuwa akitafuta sehemu Tulivu na aende Dar?
      Penye utulivu ni maeneo ya Mashambani na si mijini.
      Huyo aliamua kutafuta riziki Mijini na si sehemu tulivu.

      Agwambo Mageche.

      Delete
  2. Ni mbinu yake, alitaka watu wajue kuwa kafariki ili baada ya muda fulani iwe muujiza kuwa kafufuka. Na huenda familia ilijulishwa na ulikuwa mpango wa pamoja.

    ReplyDelete
    Replies
    1. utendaji wa kazi ya Mungu ni tofauti na mawazo ya wanadamu. YESU pia aliwahi kuondoka bila watu kujua alikokwenda na alitafutwa pia.
      GJB

      Delete
  3. hiyo ni mojawapo ya hila ya kujitafutia umaarufu

    ReplyDelete
  4. Wasiwasi wangu ni kuwa kwenye hiyo nyumba ya wageni alikutwa peke yake?

    ReplyDelete
  5. Mhh! hivyo makambako ama mkoa mzima wa Njombe usiwe na utulivu wa kuabudu mpaka uende Moro, pwani, Dar mpaka Kilimanjaro, tena bila kuaga. Mchunguzeni kwa makini huyu huenda akawa anaficha ukweli baada ya kubambwa.

    Mtu mzima alikua hajua eti sio wasia kutokuaga na imekua fundisho kwake. wazee wa kazi mfatilieni huyu kwa makini sana. Wengi walaghai wanabudu kiuzushi hapa nchi wakati yakwao yanawaendea.

    Haki kuabudu, uongo ni dhambi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli.
      Alikuwa na lake jambo si sehemu tulivu.
      Watu wengi siku hizi wanajificha kwenye dini.
      Hata Biblia inasema Wajifanya wana kondoo kumbe ni ma Mbwa mwitu wakali.

      Mageche

      Delete
  6. LENGO LAKE KUWASINGIZIA WAISLAMU KWAMBA NDIO WAMEMTEKA KWELI NI FREE MASON AGAINST ISLAM.MUNGU ATAENDELEA KUAFICHUA WAOVU.

    ReplyDelete
  7. Hivi vyombo vya habari visiripoti mambo kabla ya uchunguzi haya mlisema katekwa leo huyo kaonekana Looh hata haya hamuoni. Waandishi wengi ndio wanachochea mambo kutoeleweka hawana maadili ya kazi yao.........Hapo watu wasiopima mambo walishadhani waislamu ndo wamemteka kwanini asiage? injili inafundisha kutelekeza familia? usaniiii....

    ReplyDelete
  8. mchungaji ameleta utata na kuleta hisia mbaya ya visasi vya kidini vilivyopo sasa tanzania,pia hajui kuishi vizuri na familia kwa kutowasiliana vizuri na familia yake

    ReplyDelete
  9. Jamani! Mbona kuna simu mpaka za bure siku hizi! Kweli huyu Askofu ni feki tuuu, aliamua kuitoroka familia yake si kwa nia ya kuhubiri.

    Mlei.

    ReplyDelete
  10. Mimi sielewi,au kiswahili nimesahau,Kutiwa mbaroni ina maana kama mtu ni mvunja sheria.Ninavyofahamu mtu ana uhuru wa kwenda popota pale Tanzania bila kuhitaji visa,Swala la kutoaga mtu siyo kosa la jinai kiasi cha kumtia remand mtu mzima aliye zaidi ya miaka 18.Yesu naye alikuwa anahubiri hapa na pale. Kosa la kutoaga nyumbani ni kisingizio huku wakiwa na maana kumzuia Askofu huyo asihubiri dini yake anayoamini.Je angekuwa anahubiri dini ya serikali sasa hivi, angekematwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yesu alikua anaaaga bwana. Jifunze namna ya kuwa makini katika kuchambua mambo. Eti sio kosa kutoaga wakati anafanya kazi ya watu wengi. Kwani yeye ni shushushu ili uwepo wake usifahamike?

      Delete