02 April 2013

Askari ajeruhiwa kwa panga


Na Prosper Mgimwa,
Sumbawanga

ASKARI wa Jeshi la Polisi mkoani Rukwa amelazwa katika hospital ya mkoa baada ya kujeruhiwa kwa panga wakati akimkamata mtuhumiwa.

Tukio hilo lililotokea majira ya saa nane mchana machi 28 mwaka huu katika Kitongoji cha Katusa mjini Sumbawanga wakati askari huyo mwenye  namba
G.329D/C Rock Cosmas aliyekuwa na wenzake.

Kamanda wa polisi Mkoani Rukwa Jacob Mwaruanda  alisema kuwa askari hao mara baada ya kufika  nyumbani kwa mtuhumiwa huyo kwa lengo la kufanya  upekuzi kufuatia wizi wa bidhaa mbalimbali za dukani.

Alisema kuwa wakiwa hapo muhumiwa aligoma kufungua mlango hadi viongozi wa kitongoji walipo mbembeleza kisha kufungua huku akiwa na panga na fyreo
akiwatisha askari hao.

Kamanda Mwaruanda alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Christopher Mbilinyi (35) aliyemjeruhi kwa panga mkono wa kushoto kuvunjika ndipo askari wenzake
walijihami kwa kumpiga risasi mguuni.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuiba mali katika duka la Sumry Enterprises kufuatia wizi uliofanyika machi 27 mwaka huu ambapo askari na mtuhumiwa
wote wamelazwa katika hospitali ya mkoa huku mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

No comments:

Post a Comment