04 April 2013

Afariki dunia kwa shoti ya umeme Dar



Na Miriam Sarakikya

MKAZI wa Mbagala Sabasaba, Dar es Salaam, Saidi Madafu (33) amefariki dunia baada ya kunaswa na umeme akiwa kazini.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Engelbert Kiondo, alisema tukio hilo limetokea juzi, saa tisa alasiri maeneo ya Mtoni wakati marehemu akiwa kwenye matangazo ya Kampuni ya Tigo.

Alisema marehemu alikuwa fundi mabango ambapo siku ya tuki, yeye na mafunzi wenzake walikuwa wakiweka bango eneo la kampuni hiyo Mtoni ambalo liligusana na waya za umeme na kusababisha mlipuko ambao ulimuunguza marehemu.

“Baada ya kutokea mlipuko, marehemu alianguka chini na kufariki papo hapo ambapo mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Temeke.

Wakati huo huo,  Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni lipofanya msako mkali katika maeneo ya Manzese na kuwakamata watuhumiwa kumi ambao kati yao walipatikana na bangi puli 18,
kete 28 pamoja na pombe haramu ya ya gongo lita 40.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Charles Kenyela, alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi na kuwataka baadhi yao
kuwa ni Abubakar Abdu (28) Athumani Hamisi (31) Shukuru
Issa (26) na wenzao saba.

No comments:

Post a Comment