04 April 2013

Auawa kwa kisu akiwa muziki



Na John Gagarini, Kibaha

MFANYAKAZI wa baa ya Shimbikati, iliyopo Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, Hamis Kilongani (30), ameuawa
kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali (kisu), tumboni.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha, Mkoa wa
Pwani, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ulrich Matei, alisema marehemu alikutwa na mauti akiwa kwenye muziki na wenzake.

Alisema tukio hilo limetokea Machi 31 mwaka huu, saa tisa
usiku, katika eneo la Kiluvya B, wilayani Kisarawe.

Kamanda Matei alisema, wakati marehemu akicheza muziki na wenzake, zilitokea vurugu ambao watu wasiofahamika walimvamia na kumchoma kisu tumboni.

“Marehemu alikuwa kitengo cha chakula kwenye baa hiyo, hadi
sasa watu wawili wanashikiliwa ambao ni Max Nanyalu (32),
mkazi wa Kiluvya na Salma Salehe,” alisema.

Alisema chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika na mwili
wa marehemu umehifadhiwa kkatika Hospitali ya Taifa Muhimbili,” alisema Kamanda Matei.

No comments:

Post a Comment