26 March 2013
Tuilinde amani yetu kuvutia wawekezaji kutoka China
RAIS wa China Xi Jinping, jan alimaliza ziara yake ya siku mbili nchini na kusisitiza umuhimu wa nchi hizo, kuendeleza uhusiano uliodumu muda mrefu.
Akiwa nchini, rais huyo ameweza kuitangaza Tanzania kimataifa na kumuhakikishia Rais Jakaya Kikwete kuwa, baada ya kurejea nchini kwake, atazishawishi kampuni mbalimbali kuja kuwekeza Tanzania.
Kimsingi ziara ya kiongozi wa China ambaye nchi yake inajivunia ukuaki mkubwa wa mchumi, imeweza kuitangaza Tanzania kimataifa hasa kutokana na hotuba yake.
Hotuba hiyo aliisoma wakati akifungua Ukumbi wa Mikuitano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ambayo ilirushwa 'Live',
na kituo cha Televisheni cha China (CCTV).
Kubwa ambalo Rais Jinping amelisisitiza kwa Watanzania ni kulinda amani na utulivu uliopo ili kuvutia wawekezaji ambao watakuja kuwekeza nchini ili kuchochea maendeleo ya haraka.
Alisema mataifa mbalimbali ambayo yapo katika machafuko,
hayawezi kukuza uchumi wake kutokana na kukosa wawekezaji
ambao huofia usalama wa maisha yao na mali zao katika nchi
ambazo zimekubwa na machafuko.
Hivi karibuni, Rais Jakaya Kikwete wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Chama Cha Mpinduzi (CCM), unaofanyika
mjini Dodoma , aliwaonya watu wanaotumia mwamvuli wa
dini kutaka kuvuruga amani iliyopo nchini.
Katika mkutano huo, Rais Kikwete alisema, Serikali ipo makini kuhakikisha mtu yeyote ambaye atajaribu kuwaweka Watanzania
roho juu, atachukuliwa hatua bila kujali ni nani na anatoka wapi.
Alisema ni aibu kufanya vurugu hasa ukizingatia kuwa, Watanzania wamelelewa katika misingi ya upendo, kuheshimiana, mshikamano na uadilifu ambapo kazi hiyo ilifanywa na waasisi Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Aman Karume.
Aliongeza kuwa, vurugu zinazoendelea kutokea nchini kwa kivuli cha dini, zinachangia kuidhalilisha nchi na Watanzania kwa ujumla.
Sisi tunasema kuwa, amani ya Tanzania ndio sifa kubwa tuliyonayo katika mataifa mbalimbali duniani na ndio msingi wa kuvutia wawekezaji, ongezeko la watalii na ukuaji uchumi wa nchi.
Amani ni bidhaa adimu kuliko petroli na umeme, hatuwezi kukopa amani hivyo ni muhimu kila Mtanzania, kuilinda na kuithamini kwa nguvu zote bila kujali dini yake, kabila wala rangi.
Matukio ya hivi karibuni ya uchomaji moto kamanisa na uharibifu wa mali yaliyotokea Zanzibar, Dar es Salaam na mikoa mingine ni kielelezo cha uvunjifu wa amani hivyo Watanzania wote
tunapaswa kuunga mkono kauli ya Rais Jinping.
Imani yetu ni kwamba, vurugu zinazofanywa na baadhi ya watu wanaotumia mwamvuli wa dini kuvuruga amani ni kinyume na matakwa ya katiba ya nchi ibara ya 19(3).
Leo hii Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za kujiletea maendeleo ambazo zinahitaji utatuzi hivyo kama vurugu hizo zitaendelea, matumaini ya Watanzania kuondokana na kero walizonazo yatakuwa madogo.
Amani ya Tanzania haitadumishwa kwa ngonjera za kusema
nchi yetu ni ya amani bali jambo la msingi ni kuilinda. Tusiruhusu makundi ya watu wachache wenye uchu wa madaraka wakatupandikiza fikra za kuvunja amani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

HIVI WAKAZI WA MTWARA WANAKUELEWA AU HUTAONEKANA MAMLUKI UKIWEZA KUWASHAWISHI KUKUBALI HILO UTAPEWA UDAKTARI WA FILOSOFIA
ReplyDelete