05 March 2013

Mwalimu Mkuu Ifunda anusurika kuuawa



Na Eliasa Ally, Iringa

WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, jana walifanya vurugu kubwa shuleni hapo na kutaka kumuua Mkuu wa shule hiyo, Bw. Shaaban Nsute.

Katika vurugu hizo ambazo zilianza juzi jioni hadi saa tano usiku, wanafunzi hao ambao walivalia kininja na kuficha sura zao wakiwa na visu mkononi, walivunja vioo vya madirisha shuleni hapo.

Wanafunzi hao wanadaiwa kumfuata Bw. Nsute nyumbani kwake lakini alikimbia na kwenda kujificha kwenye shamba la mahindi ambapo wanafunzi hao walimpiga mlinzi wa shule Bw. Yasini Luhala kwa mawe akiwa katika ofisi yake.

Akizungumza na Majira jana, Bw. Nsute alisema chanzo cha
vurugu hizo ambazo zilidhibitiwa na Jeshi la Polisi ni baada ya mwanafunzi mmoja shuleni hapo kuvaa kofia zinazotumiwa na Waislamu (baraghashia).

Alisema mlinzi wa shule hiyo, Bw. Luhala alimnyang'anya
kofia hiyo ili asiingie nayo darasani kwa sababu si sare ya
shule lakini mwanafunzi huyo alichukua uamuzi wa
kwenda kuwaita wenzake na kufanya vurugu.

Aliongeza kuwa, kutokana na vurugu hizo zaidi ya wanafunzi
30 wamefukuzwa shule na kuwataja baadhi yao kuwa ni Sadi Mwamed, Jamal Hashim na Athuman Ibrahim wanosoma
kidato cha tano. Wengine ni Abdulazizi Hussein na Ally
Abdallah wanaosoma kidato cha nne.

“Mwanafunzi aliyenyang'anywa kofia alidai Waislamu katika
shule hii wanatengwa, kunyanyaswa na kuzuiwa wasifanye
mambo yanayoendana na dini yao.

“Hawa wanafunzi walikuja nyumbani kwangu usiku na kugonga mlango, nilitoka mlango wa nyuma nikakimbia kwenye shamba
la mahindi, mke wangu alifungua mlango na kuwaambia sipo
na alipowahoji wakamwambia walikuwa wakinihitaji ili
niende nao Msikitini kuna kazi muhimu,” alisema.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt Letisia Warioba, 
alisema tukio hilo limemsikitisha sana.

Alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kufika mapema eneo la tukio, kutuliza vurugu na kuimarisha ulinzi shuleni hapo hadi asubuhi
na kuwataka wanafunzi waliobaki, waendelee na masko kwa
kuzingatia taratibu za shule.

38 comments:

  1. Mungu awape uvumilivu maana kama hata Baraghashia italeta hayo, basi hata kazi nyingine hazitafanyika. Bungeni Baraghashia inaruhusiwa iwapo mtu amevaa kanzu na koti, je ndugu zetu tunataka hata dress code tofauti shuleni? Hiyo dini imeanza jana? Tunajua kuwa kuna Seminaries ambazo huko wanafunzi hujimwaga katika mambo ya dini, lakini Ifunda ni ya Serikali na ipo miaka nenda miaka rudi, kulikoni? Je hiyo Baraghashia inayoleta kizaa zaa ndiyo njia ya Mbinguni? Tutumie busara ndugu zangu

    ReplyDelete
    Replies
    1. tatizo waislamu wanapenda kujihesabia haki bila kujali majukumu!

      Delete
    2. HAKUNA WAJIBU BILA HAKI WAKIRISTO MNAJIFANYA HII TANZANIA NI YENU WE'RE TIRED.

      Delete
    3. Wewe peke yako ndio mchovu. Waislamu wenzako wanasoma na kuendesha shughuli zao bila bughuza yoyote. Ukitoka vibaya utashuhulikiwa tu. Kwa vile unaowatesa sio wakristo tu hata waislamu wenzako na wasio na dini yoyote.

      Delete
    4. Huyo jamaa anaonekana kachoka kweli, mimi nina wasiwasi na elimu yake. Inaonyesha ni kati ya wale wenye Elimu Dunia hafifu, soma kijana elimu dunia kwa saaana ili upate nguvu. Pole sana.

      Delete
  2. Ndiyo maana mitito yetu inafeli. Baada ya kufuata yaliyowaapeleka shuleni, wao wanataka wafanye mengine nje ya taratibu za shule. Laiti ningelikuwa na majukumu hayo, hao wanafunzi ningewafukuza shule jumla na gerezani wangeenda.

    ReplyDelete
  3. Sioni tatizo hapo,nadhani kutakuwa kutokuelewana kati ya mlinzi na huyo mwanafunzi,mlinzi hujatumia busara kumnyang'anya kofia kuna kamati za maadili zinafanya nini hapo shuleni.mimi mwenyewe nimesoma hapo Ifunda sidhani kama isue ilikuwa kubwa hivyo.katika kusolve isue tutumie busara hata kama unamadaraka utakapotumia nguvu ndiyo mambo kama hayo yanatokea.siku hizi siyo kama zama zile.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kama kosa ni la mlinzi amefanya kosa au hakutumia busara je mkuu wa shule na majengo ya shule navyo vinahusikaje?

      Delete
    2. watoto adabu fupi siku hizi. ni nini maana ya uniform? Uniform inaleta usawa na sura moja katika kundi, hence mazingira muafaka kwa utulivu wa shughuli iliyokusanya kundi hilo.

      elimu inashuka kwa kuwa vijana wanajichanganya na mambo mengi ambayo siyo mambo ya msingi ya uwapo wao mashuleni.

      Dawa ya makundi haya chochevu ni kuyashughulikia kama wahalifu kama kamanda mwema anavyosisitiza.

      Vijana tulieni dunia tambara bovu ukienda hovyo.

      Delete
  4. huyu mwsanafunzi aliyesababisha fujo anafaa kusoma seminary kwani ansingebuguziwa, ufahamu wake mdogo ndio chanzo cha fujo

    ReplyDelete
  5. IKO DHANA YENYE MAPUNGUFU MAKUBWA KUWA UKIWA UKO JUU "COGNITIVE" WEWE NI MTAALAMU HATA KAMA UKIWA UNA UWEZO MDOGO SANA KWENYE " PSYCHOMOTOR" NA "AFFECTIVE"

    ReplyDelete
  6. HAWA NI WALE WALE WALIOFELI MTIHANI WA FORM TWO WAKAPITISHWA WANAOGOPA KUFELI FORM FOUR WANATAKA KUFUKUZWA MAPEMA KITABU HAKIPANDI

    ReplyDelete
  7. Tatizo siobaraghashia,Tatizo kubwa nikuwa Waislamu katika Nchi hii wanadhalilishwa,wanateswa nakuonekana kuwa ni wtu wa daraja la chini kabisa .hawapewi nafasi yyte kwenye jamii hii.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Waislamu wameoa wakristo, waisilamu wanasoma na wakristo, waislamu wanafanya kazi na wakikristo, waislamu wanaongoza nchi na wakristo, waislamu wanasafri na wakristo. Lakini muislamu mmoja asioyependa amani anadhalilisha uislamu kwa kudai kua waislamu ni wa daraja la pili katika nchi hii.

      Delete
    2. Viongozi wangapi ni waisilamu? Au unaongea ili uonekane kuwa na wewe upo? Hampewi nafasi kwa sababu elimu dunia hamuijui. Na wengi waliopewa nafasi wamepewa kwa upendeleo tu.

      Delete
    3. Hakuna anayewaonea waislamu but wenyewe mnajishtukia tu kutokana na uelewa wenu pamoja na chuki mnazofundishwa dhidi ya dini zingine!

      Delete
  8. Wewe usione kama umepatiwa majibu ya mtihani ukajiona unajua saaana, wewe ni zero kabisa . Kama mnaona waislamu ni waliofeli tu basi waambieni hao mabwana zenu waweke mitihani kwa njia za DIGITAL sio majina halafu tuekewe watungaji mitihani kutoka nji ya Tanzania wasitunge hapo kanisani ,iwe imefungwa kwa sld na Itoke siku hiyo hiyo ya Mitihani ,
    TUONE SASA NANI WATAKAO FELI KATI YA WAISLAMU NA MAKAFIRI ,ACHENI ujinga nyinyi .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe inaonyesha ni mmoja wa waliofeli.

      Delete
    2. Hayo mawazo ya mtu asiye elimika, ucjidanganye wewe hakuna upendeleo wa usahihishaji kati ya waislam na wakristo, walimu tukienda kusahihisha mitihani tunakuta namba za wanafunzi na sio majina ya akina Yohana au Rashid.Tubadilike jaman,play your part soma kwa bidii u will get your reward.Waislam achen kulalamika kwenye suala la elimu jamani,there is no shortcut hapo.

      Delete
    3. wewe ni lumpen kabisa,cowdise,kwenye ulaza unaongoza kabisa,watahiniwa huwa wanaandika namba tu na si majina,inaonesha jinsi gani usivyo elimika nyamaza au nenda darasani kasome.

      Delete
    4. duuuh! kazi kwelikweli

      Delete
  9. Ubaguzi kweli uko. Wameletwa FBI kuwatafuta waliomuuwa Bishop tu na kwa baada ya siku kidogo tu akauliwa yule imamu na kabla ya hapo aliuliwa polisi muislamu lakini FBI inawahusu watu wa kanisani tu, na hapo ndipo zinapopanza fitina za kidini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Makanisa yamejaa kila kona Zanzibar, laikini hakuna wafuasi isipokuwa wale waliotoka bara tu na jamaa wanajaribu sana bila yakuvunjika moyo kuwateka waislamu, lakini wapi, kwani muislamu wa kweli habadili dini yake.

      Delete
    2. unaupungufu mkubwa katika ubongo wako,FBI WALIKUJA baada ya uhalifu kukithiri na sio udini,acha ulumpen.

      Delete
  10. NECTA WANAFANYA VIZURI KUTOONESHA MAJINA YA WATAHINIWA WANGEONESHA INGESAIDIA KUFANYA TATHINI NI NANI WANAOHUDHURIA SHULENI NA NI NANI WANAOSOMA BAADAYE UTANDAWAZI UTAWEKA WAZI NI RASILIMALIWATU IPI YENNYE SIFA YA KUPATA AJIRA KICHAA AKIIBA NGUO ZAKO UNAOPOOGA MTONI BAKIA PALE PALE MPAKA UPATE MSAMARIA WA KUKULETEA NGUO KWANI KINYUME CHAKE NI WEWE KUONEKANA KICHAA NA KICHAA KUONEKANA KUWA NA AKILI TIMAMU

    ReplyDelete
  11. tuna poelekea ni kubaya sana kwani huwa tunasahau kabisa ni vitu gani vinahitajika wakati gani.Mimi nimesoma ifunda siku za kwenda kusali tunaruhusiwa kuvaa kanzu,kofia na kwenda kuabudu lkn siku za kawaida au saa za darasani huruhusiwi kuvaa kofia aina yeyote ile ,ndala,khanga kwa hiyo mi naona ni vizuri kufuata sheria zilizopo na si vinginevyo la sivyo unatafuta sehemu ambayo unaona inakufaa kutokana na matakwa yako

    ReplyDelete
  12. kijana alishapania kutafuta shari kwa kuwa alishakatazwa asivae bargashia,nae akavaa kutishia aone mlinzi atafanya nini.mlinzi kufanya kazi yake akaleta jeshi lake.tulikofika kubaya,iman za kidini ni potofu,mawazo ya kidin ni mgando,ingekuwa shule ya kanisa ndo asingeivaa kabisa,wala kusuburu maana hawaruhusu nguo za nyumbani.nenda st anthony mbagala,hata kama wewe ni dini gani,utavaa nembo ya msalaba,hutaki,tafuta shule ingine.wanachezea shule za serikali za walipa kodi.

    ReplyDelete
  13. Jamani tusiwe na imani za kuviziana au kutafutana bali tuitafuteni mbingu au pepo.Soma biblia,Quran na Hadith tuzielewe vizuri zinataka nini,pia tuelewe mtume alifanya nini penye imani mchanganyiko.

    ReplyDelete
  14. ASILIMIA 90 YA VIONGOZI WOTE TZ WAISILAMU HATA TUME YA KATIBA.SASA HATUJUI KAMA MAWAZO YENU NDO HAYO NINI KINAENDA TOKA KWENYE KATIBA MPYA

    ReplyDelete
  15. HILI LA WANAFUNZI LIMETOKEA BAGAMOYO SEKONDARY, USAGARA, TOSAMAGANGA,LITI MOROGORO, UDOM, MUDA SI MREFU LITAANZA MAKAZINI SASA TZ ITAKUWA KAMA NIGERIA! KWA SABABU YA HIZO FIKRA MGANDO NA MAWAZO YA KUSHIKIWA NI HATARI SANA. SASA MWALIMU KUMUUA ILI WAPATE NINI, NAE NI MKRISTO HUYU? TUMIENI AKILI VIZURI SIO NGUVU TU NA MAJAMBIA

    ReplyDelete
    Replies
    1. KUNA WATU WENYE KIU YA KUMWAGA DAMU WANAOJIITA WAISLAMU. HATA KATIKA NCHI ZA KIISLAMU HAWATAKIWI VILE WANASABABISHA VIFO VINGI. WAISLAMU NA WAKRISTO TUSIWAKUBALI WATU HAO. NI WAUAJI!! SASA HUYU MWENZETU ETI ANATAKA MWL. MKUU AUAWE. KWASABABU YA YA KIBARAGHASHEE CHAKE. JAMANI!!!

      Delete
  16. AMA KWELI DUNIA SASA IMEVAA BUKTA MUDA SI MREFU ITAVUA NA KUBAKI UCHI, YAANI KIBARAGASHEE TU KITAKE KUMTOA MTU ROHO.

    ReplyDelete
  17. WAJAMENI SASA MNAPOSAJILI WANAFUNZI IWENI MAKINI MAANA INAELLEKEA HUKO TUENDAKO HATA ALKAIDA WATAJICHOMEKA MASHULENI KWA KIVULI CHA UANAFUNZI, NDIYOO MANA HAIJI AKILINI ETI KIJANA AVULIWE KIBARAGASH TU AKALETE JESHI.

    ReplyDelete
  18. Acheni siasa za kidini,hili wazo la kusema waKristo wanapendelewa na waislamu wananyanyaswa linatoka wapi?Katika nchi hii sote ni watanzania,alipouawa Padri,alipouawa immamu na askari wote hao ni Watanzania,Serikali ina wajibu wa kuzuia mauaji dhidi ya watanzania na si kwa sababau ya dini ya mtu.Wale wote wanaoingiza mambo ya kiimani katika hoja hii ya Ifunda na nyinginezo wale tu waliofilisika kiakili hebu tuone nchi hii ni yetu sote na sheria na taratibu ndizo zitzkazileta ambani na usawa.Vijana someni ni wakati wenu kofia au kanzu zinawakati wake "Elimu kwanza"

    ReplyDelete
  19. Twapaswa Kutumia busara ha hekima katika mambo yetu na hiyo ndio zawadi kubwa ya Muumba wetu. Asilaumiwe mwenye kibalaghashia tu lakini je ilikua ni kunyanganywa tu na wala asivamiwe Mkuu wa shule pasi naye kujua kosa lake nini tuchukue hili ni somo kwa wote na lazima mbadala wa matukio kama haya yafatiliwe sikusudii kuundwa tume zikaendeleza ufisadi lakini Maafisa wa wilaya na mikoa mpaka wakurugenzi wanafanya kazi gani kutekeleza wajibu wao au ndio wameshangilia nakujivunia kwa kuteuliwa na Rais. Tanzania na ya Watanzania tupendane, tuvumiliane na wala tusijengeane chuku ila haki lazima itendeke.

    ReplyDelete
  20. Kwanini mwanafunnzi uvae kofia darasani kwani ni
    sare ya shule au ndiyo uonekane tofauti na wanafunzi wengine. kwanini unataka uonekane tofauti na wenzio wakati sifa za hapo mlipo wote
    mnazo.

    ReplyDelete
  21. Jamani Huyo mwalimu Shabani Nsute ni mkristo! mbona kila kitu mnaleta udini.Tatizo kuna watu wavivu hawataki kujishughulisha wao kazi yao ni kulaumu tuu

    ReplyDelete
  22. Ee Mungu,irehemu Ifunda,lakini niulize swali,TANZANIA tunaelekera wapi?MIMI sipo

    ReplyDelete