Na Jesca Kileo
RAIS Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, kuomboleza kifo cha askari WP 2494 Koplo Elikiza ambaye amepoteza maisha kwa kugongwa na gari juzi mchana katika eneo la Bamaga, Dar es Salaam.
Koplo Elikiza aligongwa wakati akimsimamisha dereva gari ambalo alijiunga na msafara wa Rais Kikwete na kupewa amri ya kusimama badala yake akamgonga na kusababisha kifo chake.
“Nimepokea taarifa za kifo hiki kwa mshtuko na huzuni nyingi, nimejulishwa kuwa aligongwa na gari akiwa kazini katika eneo la Bamaga, Dar es Salaam, wakati akiongoza msafara rasmi.
“Ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha kwa Koplo Elikiza kupoteza maisha akiwa kazini kwenye utumishi wa jeshi lake
na nchi yake wakati Taifa bado linaendelea kuhitaji sana
nguvu kazi yake,” alisema Rais Kikwete.
Alimtaka IGP Mwema kumfikishia salamu zake kwa familia ya marehemu kuwa yupo pamoja nao.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema bado linaendelea kumsaka dereva aliyesababisha kifo cha askari huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
Tunawapa pole familia ya marehemu. Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema pepopni. Amina
ReplyDeletejamani hiv madereva wengine ni binadamu au mashetan hiv unapomsababishia kifo mtu kwa uzembe kabisa bila kujari inauma sana. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina
ReplyDelete