11 February 2013

Wastaafu wa polisi waiomba serikali iwaongezee pensheni



Na Grace Ndossa

WAASTAFU wa Jeshi la Polisi wameiomba serikali kuwaongezea fedha za pensheni kutoka laki 150,000 hadi 300,000 kwa miezi mitatu kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Wakizungumza  katika ofisi ya gazeti hili baadhi ya wastaafu ambao hawakutaka  majina yao yaandikwe gazetini walieleza kuwa fedha wanazopewa kwa sasa ni ndogo kutokana na kuwa na kupanda kwa gharama za maisha na kuwa na wategemezi.

Alisema kuwa tangu rais kikwete alipoongeza pensheni kwa wastaafu wote mpaka sasa bado hali ya maisha ni ngumu kwao na wanashindwa kumudu gharama nyingine za maisha.

"Wastaafu  hao walieleza kuwa mwanzoni walikuwa wanalipwa  sh 300,000 kwa kipindi cha miezi sita lakini kwa sasa wanapewa kwa kila baada ya miezi mitatu sh 150,000 fedha ambayo haitoshi kulingana na  gharama za maisha.

Hata hivyo waliomba rais  ajeree kauli yake kwamba tangu aliposema kuwa hataki wastaafu wapate shida, kwani wataishi kama wenzao wa Kenya na Uganda  ambao huwezi kumtofautisha na mtu anayefanya kazi.

Baadhi ya wastaafu hao walieleza kuwa  japo Rais alisema kuwa lakini hakuna kilichotendeka  bado wameendelea kubaki katika hali ambayo siyo nzuri inayowafanya  waishi kwa  matatizo na wengine kukata tamaa.

Pia walieleza kuwa kiwango cha nyongeza kilichoongezwa tangu mwaka 2009 kilikuwa ni asilimia 132 kwa mtu aliyekuwa  wa kiwango cha chini sana anapokea sh 21,601, hadi kufikia kiwango cha sh. 50,144



No comments:

Post a Comment