11 February 2013

Ilala walalamikiwa kuwa chanzo cha uchafu soko la Kibasila


Na Veronica Ikonga

HALMASHAURI ya Wilaya ya Ilala amedaiwa kuwa ni chanzo cha kuwepo kwa uchafu katika soko la Kibasila Dar es Salaam kutokana na kutotoa uchafu kwa wakati.

Akizungumza na gazeti hili mweka hazina wa soko hilo Ramadhani Kisiigalile alisema chanzo cha uchafu huo kuwa mwingi ni kutokana na halmashauri kutofika katika eneo hilo kusomba taka kwa wakati unaotakiwa.

Alisema magari halmashauri yanatakiwa kufika kila baada ya siku tatu hadi nne sasa badala yake wanakwenda mwezi hadi mwezi hivyo kusababisha  uchafu kuwa mwingi na kikwazo kwa wateja wanaofika katika soko hilo.

Alisema kwamba watajitahadi kwa hali na mali kuwasiliana na halmashauri hiyo ambayo ndio wahusika wakuu wa tatizo hilo ili waweze kusafisha mazingira ya soko hilo.

Aliongeza kuwa na kwa wale wafanyabiashara ambao wanauza bidhaa zao kandokando ya achafu huo atajitahidi kuwatengea eneo maalum kwa ajili ya kuifadhia bidhaa zao ili kuepukana na hatari za milipuko ya magonjwa.

No comments:

Post a Comment