08 February 2013
Wanaovaa 'nusu uchi' Temeke kukiona *DC ataka wachapwe viboko ili kulinda maadili
David John na Andrew Ignas
MKUU wa Wiliya ya Temeke, Dar es Salaam, Bi. Sophia Mjema, amewaagiza Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Maofisa Watendaji wote wilayani humo, kuwachapa viboko wanawake na wanaume wanaovaa nusu uchi ili kulinda maadili ya Kitanzania.
Bi. Mjema alitoa agizo hilo Dar es Salaam jana alipofanya ziara katika Kata ya Keko, Tarafa ya Chang'ombe wilayani humo ili kusikiliza kero na wananchi na changamoto walizonazo watendaji.
Ziara hiyo ni moja ya mikakati aliyojiwekea ya kutembelea kata
zote wilayani humo. Bi. Mjema aliwataka viongozi wa kata hiyo, kutofumbai macho kuhakikisha wananchi wanaowaongoza,
wanajiheshimu kwa kuvaa mavazi ya heshima.
“Mnapowakuta wanawake na wanaume wanaovaa nusu uchi, muwachukulia hatua kwa kuwapa adhabu ya viboko pamoja
na kuwafikisha mahakamani ili iwe fundisho kwa wengine.
“Msiwe na hofu ya kuchukua uamuzi huo sheria zinazowalinda
zipo na mkikwama, mripoti maara moja katika ofisi yangu...nyie
ni viongozi wa Serikali katika kata hivyo lazima tuwe na Taifa
linalozingatia maadili,” alisema Bi. Mjema.
Aliongeza kuwa, kama hali hiyo isipodhibitiwa mapema Taifa litakuwa na vijana legelege, makahaba, majangili, makaka poa
pamoja na ongezeko la machangudoa jambo ambalo ni hatari.
Katika hatua nyingine, Bi. Mjema aliwaagiza viongozi hao kuhakikisha wanafunzi wanaokaa katika magenge ya wahuni
na kumbi za starehe badala ya kwenda shule, wanakamatwa, kuchapwa viboko na kupelekwa shule kwa lazima.
“Mkiwakamata kwanza wachapeni viboko, kuwapa elimu ili
watambue umuhimu wa kusoma na kuwapeleka katika shule
zao, hatuwezi kuruhusu wazurure hovyo mitaani na kucheza
kamali huku ni kuzalisha bomu kubwa kwa Taifa,” alisema.
Aliwataka Maofisa Watendaji wote kutotoa vibari kwa vikundi mbalimbali vinavyopiga muziki masaa 24 na kusababisha wananchi kutopata muda mzuri wa kupumzisha akiri zao baada ya kazi.
“Katika baadhi ya maeneo yanayopiga muziki masaa 24, jirani zao ni wagonujwa lakini wahusika wamepewa vibali...kuanzia leo vibari vyote vya aina hii vipitie kwangu ili kuona kama kuna ulazima wa kufanya hivyo,” alisema.
Alisema baa zote zinazofunguliwa kuanzia saa nne asubuhi ni marufuku kwani muda huo ni wa kazi kwa kila mwananchi
ambaye anapaswa kujitafutia siziki si vinginevyo.
Aliongeza kuwa, wamiliki wa baa ambao watakiuka agizo hilo watachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani
ambapo watendaji wote, wasitoe vibari vya kuruhusu hali hiyo.
Bi. Mjema alisema umefika wakati wa viongozi kufuata utawala
wa sheria ili kuepusha malalamiko kutoka kwa wananchi hivyo kuazia sasa, aliwataka Watendaji wote, Wenyeviti na idara
zingine kufanya kazi kwa kuzingatia utawala bora.
“Toeni taarifa ya mapato na matumizi katika vikao hasa vinavyoshirikisha wananchi ili kuepusha migongano na lawama zisozo na msingi lakini kubwa zaidi ni kuacha kuwalipisha
wananchi fedha ambazo kisheria hazipo pindi wanapohitaji
mihuri na kuandikiwa barua za mahitaji mbalimbali,” alisema.
Katika ziara hiyo, Bi. Mjema alitembelea kata mbili ambazo
Keko, Kurasini na baadaye atatembelea kata zingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
It may not work, but I like and appreciate the guts
ReplyDeleteVIJANA WENGI WANAVUTA BANGI,MATEJA NA WASAGAJI USILOGWE UKAWAPA RUNGU BUSARA NA HEKIMA NI SIFURI WATAUA WENZAO SI VEMA KUWARUHUSU WACHUKUE SHERIA MIKONONI
ReplyDeleteHuyu DC ahamie Afganistan kwa Matalibani wenzake.Wananchi wa Tanganyika siyo Waislamu wote wanaobidi kuvaa baibui kuficha sura zao. Tuache ubabe wa Kiume wa kuwaona wanawake kwa jicho la kufanya nao NGONO tu. Wanawake ni watu wazima na wanahaki ya kuamua waendeshaje maisha yao. CCM sasa imepoteza lengo!!
ReplyDeleteHapa CCM INAHUSIKA NA NINI. Kwani huu mkakati umeuona kwenye master plan ya CCM? Au ni ubunifu wa huyu DC. Cha mhimu ni kufikiria njia ya kuboresha wazo lake na kuona kama linafaa. Tusiwe watu wa kuchallenge kila kitu
ReplyDeleteNi kweli Duniani pote zipo Mila na desturi. Kama Watanzania ni vema tuone jambo lipi kwetu ni zuri???
ReplyDeleteHivyo Viboko ni vema sana vitumike hata huku Dodoma-Geita-Mwanza. Maana wanao iga ni Wehu na daw ni Kuwacharaza kabisa.
Kuwacharazabakora mh haijakaa vizuri,kutembea uchi ni kinyume cha sheria ya nchi wala sio suala la kidini peke yake,sasa mimi kwa mtazamo wangu ni kwamba wakamatwe wachukuliwe hatua za kisheria,mikwaju inaweza ikazaa tatizo lingine kubwa pengine zaidi ya hilo.
ReplyDelete