08 February 2013

Msuya apelekwa Uingereza kutibiwa



Na Rehema Maigala

WAZIRI Mkuu mstaafu, Bw. Cleopa Msuya, amesafirishwa
juzi kwenda nchini Uingereza kwa matibabu zaidi ya mguu.


Bw. Msuya alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MNH), kitengo cha Taasisi ya Mifupa (MOI), akipatiwa matibabu.

Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Msemaji wa MOI, Bw. Almas Jumaa, alisema Bw. Msuya alilazwa katika kitengo hicho tangu Februari 4 mwaka huu na alisafirishwa juzi saa mbili usiku kwenda nchini humo akisumbuliwa zaidi na mguu.

Alisema akiwa katika kitengo hicho, Bw. Msuya alikuwa akipatiwa matibabu na jopo la madaktari Bingwa wa mifupa.

Bw. Msuya ambaye alikuwa mwanasiasa mkongwe na maarufu nchini, alizaliwa Novemba 4,1931. Aliwahi kushika nafasi nyingi serikalini ikiwemo Waziri Mkuu.

2 comments:

  1. kwanini apelekwe Uingereza na lugha yake ilikuwa chafu kwa Watanzania?alituambia kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe wakati anajua hali za wtanzania zilikuwa taabani huyu Mungu amuone kwa namna yake

    ReplyDelete
  2. KWELI JAMII FORUM NI VICHAA KUMBE NDIO SABABU MAKABURI MENGI NI YA VIJANA KW TAARIFA YAKO ZUZU HUYU HAKUWA WAZIRI WA FEDHA TU ALIKUWA WAZIRI MKUU VIPINDI VIWILI NIKUPE TAARIFA TU ; NOVEMBA1980 HADI FEBRUARI 1983 NA DESEMBA 1994 HADI NOVEMBA 1995 HIVI WEWE ZUZU UNAELEWA SHETANI MKUBWA SI UFE WEWE

    ReplyDelete