11 February 2013

Vivutio saba vya asili kutangazwa Arusha


Na Grace Ndossa

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kutangaza vivutio saba vya asili Barani Afrika zitakazofanyika Mkoani Arusha Febuari 11 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana  ilieleza kuwa sherehe hizo zitahudhuriwa na rais wa Taasisi  inayoendesha shindano hilo  la kutafuta maajabu hayo Dkt. Philip IMler kutoka Marekani .

Pia ileleza kuwa  nchi mbali mbali  Barani Afrika zitashiriki katika sherehe hizo na tayari zimeshadhibitisha ni kama Bostwana, Uganda na Zambia zimekwisha.

Hata hivyo  Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hapa nchini, baadhi ya wabunge na viongozi wengine wa kada mbalimbali wanatarajiwa pia kuhudhuria.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Sherehe hizo zinatarajiwa kuambatana na burudani ya bendi ya Mpoto, Kikundi cha Sanaa cha JKT Oljoro na vikundi vingine vya ngoma kutoka jamii ya Wamasai na watatoga.

"Katika shindano hilo ambalo vivutio kumi na mbi (12) barani Afrika vilipigiwa kura na mamilioni ya watu kote duniani, Tanzania ilikuwa na vivutio vitatu vilivyoingia kwenye kinyanganyiro hicho ambavyo ni Mlima wa Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na wanyama wanaohama katika hifadhi ya Taifa ya Seregeti,"ilieleza taarifa hiyo.

Taasisi ya  vivutio saba  barani Afrika  imekwisha taja Tanzania kuwa miongoni mwa washindi ambao  kivutio kimoja ama zaidi vimeshinda, hivyo vitaingizwa katika orodha ya maajabu Saba ya Asili ya Afrika.

Hata hiyo matayarisho ya sherehe  hizo yanaendelea vizuri chini ya Kamati ya Kitaifa inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw.Magesa Mulongo



No comments:

Post a Comment