21 February 2013

Snura kuachia video ya MajangaNa Mayasa Mariwata

MSANII wa miondoko ya mduara na filamu nchini Snura Mushi, ametoa video ya wimbo wake mpya wa Majanga.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi, msanii huyo alisema video hiyo ameitengeneza kwa umahiri mkubwa ambao mashabiki wake wataifurahia.

Alisema katika video hiyo ameonesha uwezo wake wa kukata mauno, ambayo yatawafanya mashabiki wake na wasanii wenzake kupata uhondo wa hali ya juu.

"Naamini hakuna anayenifikia kwa kipaji nilichonacho na wengi walishuhudia niliyoyafanya kwenye video ya Debe la vanga, ila kwenye Majanga nitafanya zaidi ya vile," alisema.

Alisema video hiyo anatarajia kuiachia hivi karibuni na kuwataka mashabiki wa mduara, wakae mkao wa kula.

Aliongeza kuwa yeye hapendi kumshirikisha mtu kwenye kazi zake kwa sasa, ila huenda akafanya hivyo  ili kuongeza ladha ya kazi.

No comments:

Post a Comment