21 February 2013

Chanel Africa yaitambia Mbao FCAfrica Na Daud Magesa, Mwanza

TIMU ya soka ya Chanel Africa, imeanza kwa kishindo Ligi Daraja  la Tatu Mkoa wa Mwanza, kwa kuigagadua Mbao FC mabao 2-0.


Mwamuzi Mathew Akrama, aliwatoa nje kwa kadi nyekundu wachezaji wa Chanel, Shaaban Ramadhan na Masala Stephen dakika za 42 na 43 kutokana na mchezo mbaya.

Pamoja na kucheza pungufu, Chanel ilikianza kipindi cha pili kwa nguvu na kufanikiwa kuzima mashambulizi ya Mbao FC, huku wakijenga mashambulizi ya kushtukiza langoni mwa wapinzani wao.

Wakicheza pungufu, Chanel walifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika 43 kupitia kwa Hussein Salehe, kabla ya Hassan Issa kupachika bao la pili na la ushindi dakika ya 83.

Wakati jahazi la Mbao FC likiwa limezama baada ya kufungwa bao la pili ambalo liliwanyong’onyeza, dakika ya 84 mchezaji wake Isaack Mussa, alipewa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.

Katika mechi ya fungua dimba, 
kwenye Uwanja wa Nyamagana wenyeji Nyamagana United walilazimishwa sare ya mabao 3-3 na Masabuda.
 
ends......Masabuda ya wilayani Magu, ilitangulia kupata bao dakika ya 16 ya mchezo kupitia kwa George Matei, kabla ya kuongeza la pili dakika ya 36.

Nyamagana United wakicheza kwa uelewano mkubwa walipata bao  kwa njia ya penati dakika tano kabla ya mapumziko, likipachikwa wavuni na Dickson Isaack.Penati hiyo lilisababishwa na Komba John baada ya kumkwatua mchezaji wa Nyamagana ndani ya eneo la adhabu.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Masabuda kujipatia bao dakika moja tangu kuanza kwa kipindi hicho kuptia kwa Haji Juma.

Nyamagana walitulia na kusukuma mashambulizi langoni mwa wapinzani wake na kufanikiwa kupata bao dakika ya 56 ya mchezo lililopachikwa kimiani na Musa Nyangi.

Masabuda baada ya kuongoza kwa mabao 3-2, ilipata pigo dakika ya 67 pale mchezaji wake Komba John, alipotolewa nje ya mchezo kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano na mwamuzi Alex Mahagi, aliyeekuw akisaidwaa na Livingstone Rwiza na Mbilinyi.

Pamoja na kucheza pungufu bado Masabuda  waliendelea kuwapa taabu Nyamagana United ambao walikuwa wakitafuta bao la kusawazisha, lakini makosa yaliyofanywa na wachezaji wa Masabuda ya kupoteza muda yaliwagharimu.


Matuamaini yao ya kuondoka na pointi zote tatu  yalifutwa na Musa Nyangi baada ya kuisawazishia timu yake ya Nyamagana bao ikiwa imesalia dakika moja mpira kwisha na kudabnya matokeo kuwa 3-3.

Leo katika kituo cha Nyamagana FC Jonas itakuwa inakwaana na Mwanza United katika mfululizo wa michuano ya ligi hiyo iliyopangwa katika vituo vitatu vya Nansio Ukerewe na Sengerema.

No comments:

Post a Comment