11 February 2013
Serikali kuchukua hatua mbalimbali za kisera
Mariam Mziwanda na Grace Ndosa
SERIKALI imesema kuwa itahakikisha inachukua hatua mbalimbali za kisera kupitia sheria za kodi na kupambana na watu wanaotumia fedha za serikali kujinufaisha katika vyanzo vyake vya uchumi.
Naibu waziri wa Fedha Bi.Saada Salum aliyasema hayo jana mjini Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge wa Same mashariki, Bi. Anne Kilango(CCM)lililokuwa likitka kujua mipango ya Serikali kuhakikisha wanapambana na viongozi wasio waadilifu wanaotumia fedha za serikali kujinufaisha wenyewe kama ambavyo oparesheni iliyofanyika Bandarini ilivyobainisha.
Bi. Salum alisema kuwa serikali kupitia wizara mbalimbali imejipanga kuhakikisha inadhibiti njia zote za ufujishaji wa fedha za serikali na kuondoa viongozi wote ambao siyo waadilifu.
Alisema kuwa pamoja na mikakati hiyo Serikali kupitia Mamlaka ya kodi TRA inampango wa kuimarisha uchumi kwa kudhibiti vyanzo vya mapato vya ndani kwa kutumia vitambulisho vya uraia ambavyo vitaongeza ufanisi, hivyo kuwataka wananchi kuongeza ushirikiano wa utambuzi kwa wafanyabiashara nchini.
Mbunge wa Mji Mkongwe Zanzibar (CUF),Bw. Mohamed Hamid Sanya alihoji ni kwanini Viongozi wakuu wa Nchi mbali mbali wanaowasili nchini hawatembelea zanzibar?
Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje Naibu Waziri wa Mawasilinao sayansi na Teknolojia Bw. Januari Makamba alisema kuwa viongozi wanaotembelea nchini wanamaamuzi yao wenyewe na serikali haina maamuzi ya kuwaingilia katika kutembelea sehemu nyingine ya nchi.
Pia alisema kuwa uamuzi wa kudhuru Zanzibar uko mikononi mwa viongozi hao wenyewe na kusisitiza kuwa muungano utaendelea kuimarika na hauwezi kutikiswa kwa matakwa ya wageni kutokutembelea Zanzibar.
Naye Mbunge wa Viti maalum (CHADEMA) Bi. Grace Kihwelu alihoji nini mikakati ya serikali katika kuboresha vituo vya afya vilivyoanzishwa na wananchi lakini havifanyi kazi na wananchi kueandelea kukosa huduma?
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Tamisemi Bw. Aggrey Mwandri alisema kuwa viongozi wa sekta mbali mbali wameshakutana na kuazimia kufanya usajili wa vituo hivyo na kuagiza makatibu tawala wa Mikoa kuhakikisha watumishi wanaopangiwa katika vituo vyao vya kazi wanaripoti sehemu walizopangiwa
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA)Lucy Uwenya alihoji ni lini vyombo vya serikali vitatoa fursa kwa walemavu kupata habari ikiwemo kuweka wakalimani ili kuwapatia haki hiyo ya msingi?.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Bw. Amos Makalla alisema kuwa tayari serikali imeshakamilisha sheria ya kuvitaka vyombo vya habari kuwa na wakalimani.
Pia aliongeza kuwa sheria hiyo imeshapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali ili aweze kupitisha na kutolewa kwenye gazeti la serikali na kila chombo cha habari kitatakiwa kutekeleza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment