11 February 2013
Polisi tumieni elimu, ujuzi kwa vitendo-IGP
Na Gladness Theonest
JESHI la Polisi nchini limetakiwa kutumia elimu na ujuzi kwa vitendo kwa mifano iliyo hai kwa umma na kuwa walimu na waelekekezaji kwa askari wenzao katika vitu vya kazi ili kuleta mabadiliko.
Hayo yemeelezwa jana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema kwenye maafali ya kwanza ya vyuo vya taaluma ya polisi yaliyofanyika katika chuo cha polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa upolisi ni taaluma kama taaluma nyingine inayohitaji ujuzi na maarifa ya hali ya juu kutokana na kwamba waharifu ubadili mbinu za uharifu mara kwa mara na kwa kadri muda unavyokwenda.
"Taaluma zetu ziwe ni chemchem za elimu, maarifa na ujuzi stadi ili kuwawezesha askari polisi kukabiliana na changamoto na mbinu malimbali za uharifu," alisema Mwema.
Ameongeza kuwa jesho la polisi kwa siku za usoni imeweka mipango ya kuongeza wadahiliwa kila mwaka, ambapo askari polisi atakuwa na fursa ya kujiunga na kozi hizo, mbapo mwisho wa mafunzo hayo yatakuwa ni vigezo muhimu vya kufikiriwa katika kupandishwa vyeo kwenye ngazi mbalimbali.
Naye mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho, Pro. Florence Luoga amesema kuwa lengo la kuanzisha kwa mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa taaluma za polisi zinaongezeka na mafunzo ya ngazi za juu za elimu zinaanzishwa hadi ngazi ya Phd.
Wakufunzi wapatao 416 wa jeshi la polisi kutoka katika vyuo vya polisi vya Dar es salaa, Kidatu, Zanzibar na Moshi walitunukiwa vyeti mbalimbali katika ngazi mbalimbali.
Ikiwemo stashahada ya sayansi ya polisi, cheti cha upelelezi wa taaluma ya makosa ya jinai, cheti cha sayansi ya polisi, pamoja na cheti cha taaluma ya mawasiliano ya polisi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment