11 February 2013
Hakuna hati ya makubaliano-Fasjet
Na David John.
MWENYEKITI wa Kampuni ya Ndege ya Fastjet David Leinigat amethibisha kwamba hakuna hati ya makubaliano ya Leseni au makubaliano mengine yeyote kati ya shirika la ndege la Fastjet na Fly 540 Kenya au mashirika mengine rafiki ya Fly 540 barani Afrika.
Kwamujibu wa Taarifa zilizotolewa Dar es Salaam jana na Meneja uhusiano wa Fastjet Jean Uku alisema kuwa madai ya mkurugenzi wa Fly 540 Don Smith kwamba anahaki ya kubatilisha jina na Leseni ya Fastjet hayana ukweli wowote.
"Bodi ya wakurugenzi ya Fly 540 Kenya haijawahi kukutana wala kufikilia jambo hilo na wakurugezni wengine wamethibitisha hivyo kuwa hawajajadili masuala ya yanayohusu Leseni wala jina la Fastjet"alisema Uku.
Aliongeza kuwa Fastjet ingependa kuwafahamisha vyombo vya habari na wateja wa shirika hilo wanaotumia ndege za Fastjet, Fly 540 au Fly Afrika kwamba Shirika linatarajia kupanua wigo wa ndege za gharama nafuu barani kote Afrika.
Alisema kuwa kufikia sasa wameweza kuhudumia wateja laki moja, ambapo asilimia 30 wamelipa nauli sh.32,000 ambayo ndiyo malipo nafuu ya shirika hilo.
Alisisitiza kuwa ndege zao zinakwenda kwa wakati na bila kuahirisha safari zao hivyo wananchi waendelee kuamini na kutumia huduma zinazotolewa na Fastjet.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment