11 February 2013
Naombeni msaada mtoto wangu akatibiwe India
Na Miriam Sarakikya
MKAZI wa Kijiji cha Malambene Wilaya ya Mkuranga nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam, Bw.Rashiri Mchanjoka anaomba msaada ili mtoto wake Hamisi Mchanjoka kupelekwa India kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa moyo unaomsumbua mtoto huyo.
Akizungumza na Majira baba wa mtoto huyo alisema mtoto huyo mwenye umri wa miaka (13) anasumbuliwa na ugonjwa huo wa moyo, ambapo moyo wa mtoto huyo hujaa maji kwa muda wa miaka 9 bila kupata matibabu.
Bw. Mchanjoka alisema kuwa mtoto huyo alianza kuugua akiwa na miaka 5 nakupelekwa katika Hospitali ya Muhimbili,ambapo mzazi wa mtoto huyo aliambiwa ampeleke kilniki ya watoto na yeye akafanya kama alivyoagizwa na uongozi wa hospitali hiyo.
Aidha baba wa mtoto huyo alisema kuwa akiwa anampeleka mtoto huyo kiliniki hiyo ya Muhimbili mtoto huyo akuweza kupewa dawa wala msaada wowote ambapo aliendelea kuugua na hata kumfanya akose nguvu za kuudhuria Shule.
Hata hivyo mtoto huyo ameweza kuzungumza na gazeti hili ambapo amewaomba wasamaria wema kumpatia msaada wa kuweza kupata matibabu.
"Naomba msaada wenu iliniweze kupata matibabu na niweze kuendelea na masomo, kwani nimeacha shule tangu mwaka 2009 na wazazi wangu hawana uwezo wa kunipatia matibabu hayo," alisema mtoto huyo Hamisi Mchanjoka.
Bw.Rashiri ameomba wasamaria wema kumchangia kupitia namba za simu ambazo ni za watoto wake 0714 810635 au 0719 629815.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment