11 February 2013
Mwaka mpya wa China kufanyika leo
Leah Daudi na
christina Mokimirya.
BALOZI wa China leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya kusherekea mwaka mpya wa china itakayo fanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mwalimu wa kiswahili wa Chuo Kikuu cha Kiswahili China Au Mayun alisema wameamua kufanya sherehe hiyo nchini Tanzania ili kushirikiana na watanzania ikiwa ni sehemu ya kuonyesha amani na upendo.
"Nia na madhumuni ni kukutana pamoja na watanzania kwani ni nchi ambayo tunashirikiana katika mambo mbalimbali hivyo tumeamua nasi kuwashirikisha katika jambo hili,"alisema.
Alisema sherehe hiyo itafanyika Dar es Salaam katika viwanja vya mnazi mmoja ambapo kutakuwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Tanzania.
Pia aliwataka viongozi wa Tanzania kuonyesha ushirikiano katika nchi mbalimbali kwani ni sehemu ya kuijengea amani nchi ya Tanzania.
Aidha alisema kuwa katika sherehe hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali ambazo zitaboresha na kusindikiza sherehe hiyo.
Mayuni alisema kuwa watakuwepo wanafunzi mbalimbali wa china ambao wako Tanzania na watapewa fursa ya kuimba wimbo wa Tanzania kwa lugha ya kiswahili na wengine wa Tanzania ambao wanaishi china nao watapewa fursa ya kuimba wimbo wa china kwa lugha ya china.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment