18 February 2013
Minara ya Vodacom 3G yavutia wateja
Na Mwandishi Wetu
ZAIDI ya wakazi 200 waishio katika maeneo ya Mwananyamala
na Kinondoni, Dar es Salaam, jana walijitokeza kushuhudia kampeni inayoratibiwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania ya kuhamasisha umma kuhusu mageuzi ya teknolojia kupitia minara mipya ya 3G.
Minara hiyo imefungwa katika maeneo hayo ili kutoa kwa wateja
wa kampuni hiyo kupiga simu na kupata huduma za kupiga simu pamoja na kupata intaneti kwa haraka zaidi.
Akiongoza utekelezwaji wa kampeni hiyo, kiongozi wa timu
ya mauzo kutoka kampuni hiyo, Sade Acuncion, alisema amefurahishwa na mwitikio wa wakazi wa jiji hilo jinsi
walivyoyapokea mabadiliko hayo ya teknolojia.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kampeni hiyo, walisema wamefurahishwa na kampuni hiyo kusogeza na kurahisisha upatikanaji huduma za kila siku kupitia mtandao huo.
“Minara hii ni mizuri, intaneti yangu tangu nilipounganishwa haisumbui kama mwanzo ila nawaomba waongeze ofa zaidi ili
wateja tuweze kunufaika maradufu,” alisema Bi. Khadija Mrope
mkazi wa Mwananyamala.
Pamoja na kampuni hiyo kutoa elimu inayohusu matumizi ya minaara hiyo, wateja wa mtandao huo kuzunguka maeneo mbalimbali ya Mwananyamala wamepatiwa simcard za
bure pamoja na usajili wa huduma ya M-Pesa.
“Ni hatua nyingine muhimu kutoka Vodacom tunapowawezesha wateja wetu kupata huduma bora sokoni bila mabadiliko ya
gharama,” alisema Mkurugenzi wa Vodacom nchini, Bw. Rene Meza, wakati akizundua minara hiyo hivi karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment