01 February 2013

Mbatia alitikisa Bunge Dodoma *Ni kuhusu hoja ya udhaifu sekta ya elimu *Wabunge wa CHADEMA, CCM wavutana



Rose Itono na Goodluck Hongo

MBUNGE wa kuteuliwa kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, jana aliwasilisha hoja binafsi iliyoainisha suala zima la udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini.

Alisema kukosekana kwa mitaala katika shule za msingi na sekondari kunachangia wanafunzi kufanya vibaya na utendaji
mbovu wa kitengo cha kuandaa mitaala hiyo, kimeshindwa
kufanya kazi zake ipasavyo na kusababisha usambazaji
vitabu kunuka harufu ya rushwa.

Hoja hiyo iliyoibua mvutano mkali wa wabunge, iliwasilishwa bungeni mjini Dodoma. Baadhi ya wabunge walishauri iundwe
Kamati Teule ya Bunge kuchukuza udhaifu huo na wengine
wakitaka hoja hiyo ifanyiwe kazi na Serikali.

Kutokana na hali hiyo, Spika wa Bunge Bi. Anne Makinda alilazimika kusimama na kujibu hoja za wabunge lakini kambi
ya upinzani ilikuwa na msimamo wa kutaka iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchunguza udhaifu ulioainishwa na Bw. Mbatia.

Wabunge wa CCM walipinga msimamo wa kambi ya upinzani
na kutaka hoja hiyo ifanyiwe kazi na Serikali wakidai Bw. Mbatia ameainisha mambo mengi ambayo kaamati haiwezi kuyafuatilia
kwa wakati mmoja yakiwemo ya kisera.

Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Simanjiro, mkoani Manyara,
Bw. Christopher Ole Sendeka (CCM), alishauri hoja hiyo iachewe Serikali na kusisitiza kuwa, kikanuni kazi ya kuunda Kamati Teule hasa kwa suala la elimu linahitaji ujuzi na utaalamu wa hali ya juu.

“Japo kuwa wabunge ni wasomi, hakuna ambaye ni mtaalamu wa masuala hayo hivyo jambo hili liachiwe Serikali ifanyie kazi hoja
ambazo zimewasilishwa na Bw. Mbatia,” alisema.

Mbunge wa Arumeru Mashariki, mkoani Arusha Bw. Joshua Nassari (CHADEMA), alisema inaonekana wabunge wameanza kukimbia majukumu ya kibunge kwa kukataa tume hiyo isiundwe.

Alisema kazi kubwa ya wabunge ni kuisimamia Serikali ambayo haiwezi kujisimamia yenyewe. “Katika Bunge hili, iliungwa Kamati Teule ikiongozwa na Dkt. Harrison Mwakyembe, kuchunguza sakata la Richmond...” alisema Bw. Nassari.

Mbunge wa Peramiho, mkoani Ruvuma, Bi. Jenista Mhagama (CCM), alisema kwa mtazamo wake wabunge wote wanajenga nyumba moja hivyo jambo la msingi ni kuangalia namna ya
kuiboresha hiyo iweze kufanya kazi zake vizuri.

Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), alisema elimu ni gharama hivyo lazima madudu yaliyomo ndani
ya sekta hiyo yaondolewe na kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

“Hoja aliyoitoa Bw. Mbatia ni ya msingi kwani elimu ni gharama kubwa hivyo lazima ijadiliwe kiundani na kukokotoa madudu yote, kazi ya bunge ni kuisimamia Serikali si vinginevyo,” alisema na kuongeza kuwa, kamwe Serikali haiwezi kujichunguza yenyewe.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, alisema Serikali imezingatia hoja zilizotolewa na Bw. Mbatia na kuahisi kuifanyia kazi ambapo hivi sasa wapo katika mapitio ya
sera ambayo yamechukua muda mrefu.

“Ieleweke kuwa, kuna mambo makubwa yanapaswa kuangaliwa ili ifikapo 2020, Taifa liweze kufikia hadhi ya kimataifa,” alisema.

Katika hoja yake, Bw. Mbatia alidai pamoja na mambo mengine, kuna kasoro nyingi kwenye mitaala wakati mwingine mtuzi wa vitabu anageuka kuwa Mhariri jambo ambalo si sahihi.

9 comments:

  1. MBATIA UNAJENGAJE HOJA BILA KUWA NA MITAALA HAINGII AKILINI USEME MITAALA HAIPO INAPOONESHWA USEME UNAIOMBA ILI UJENGE HOJA UPYA HALAFU WAPINZANI WANATOKA NJE YA BUNGE NI UTAMADADUNI WA KIPUUZI SANA

    ReplyDelete
    Replies
    1. WEWE NDUGU YANGU SIJUI WEWE UNAISHI WAPI, NA ULISOMA WAPI, ILA SUALA LA SYLABUS/MTAALA WA ELIMU YA MTANZANIA HAUKIDHI MAHITAJI YA MTANZANIA. LEO HII NINGEKTANA NA WAZIRI MMOJA NINGEMUAMBIA KWAMBA MIMI NI NABII. TULIKUWA WATANZANIA WENGI SEHEMU NA HILI SUALA LA ELIMU NILILIONGELEA NI PROFESER HAKUWA NA POINT YOYOTE YA KUNIPINGA. KWA HIYO ELIMU YETU YA TANZANIA BADO IKO CHINI WALA HAIKIDHI VIWANGO VYA KIMATAIFA.TUNASIKIA IDADI YA WATU INAONGEZEKA JE NI KWA JINSI GANI TUNAWAANDAA HAWA WATU KWA MIAKA IJAYO WAWEZE KUFANYA KAZI SEHEMU MBALI MBALI DUNIANI? ULAYA NA AMERIKA WATU HAWAZAI TENA SISI AMABAO TUNAWATU NI RESSOURCES TAYARI HOW DO WE USE THIS RESOURCES? KAMA UNATAKA KUINUAMA MAISHA YA MTANZANIA WAPATIE ELIMU. ANGALIA NDUGU ZETU WAKENYE WANAMALIZA FORM 4 WANAINGIA CHUO KIKUU? JE TANZANIA KUNA MWANAFUNZI ANAYETOKA FORM 4 ANAWEZA INGIA CHUO KIKUU? KUIFANYA TU RAHISI KUANDIKA BARUA YA MAOMBI YA KAZI NDIYO UTAJUA KWAMBA WE STILL HAVE A LONG WAY TO GO. KAMA JINSI TUNAVYOHITAJI KATIBA MPYA PIA SUALA LA ELIMU NI LA KUFANYIA KAZI? MTU ANAYETOKA CHUO KIKKUU TANZANIA AWE NA UJUZI SAWA NA MTU ALIYESOMA CHUO KIKUU CHA OXFORD AU VYUO VINGINE

      Delete
    2. MTAALA SIO SYLABUS ILA MTAALA HUTUMIKA KUUNDA SYLABUS NI UPOTOSHAJI KUSEMA MTAALA HAUPO HIYO NI SERA IPO NA INATUMIKA KUUNDA MIHUTASARI WALIOFANYA NCHI IYUMBE KIELIMU NI WALIOBABILISHA SERA BILA MTAALA AWALI KATIBA ILITAMKA TUTAJENGA NCHI YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA SERA YA ELIMU ILIKUWA ELIMU YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA [AZIMIO LA ARUSHA] LEO NI AZIMIO LA ZANZIBAR SOKO HOLELA JE SERA YA ELIMU NI IPI MTAALA NI UPI USIOENDANA NA SERA YA AZIMIO LA ZANZIBAR KUMBUKA MTAALA UNAHUSU YAFUNDISHWAYO DARASANI NA NJE YA DARASA SINA UHAKIKA WABUNGE HAWA[HOUSE OF COMMONS] WANA UELEWA HUO

      Delete
  2. Ndugu zangu Watanzania.. ebu tufikiri kwa upana zaidi na tuendelee kutafuta sababu nyingine zinazofanya elimu kushuka kuliko kuona mitaala ndio sababu ya mwisho na ikitatuliwa basi mambo yatakuwa mazuri. Kwani shule za binafsi especial seminary zinatumia nn na je miongoni mwa shule za kata hawapo watoto wanao fanya vzr? MAPENDEKEZO YANGU: Hebu tuvichunguze vipengele vifuatavyo;
    1. Mchango wa wazazi kwa watoto wao wawapo majumbani
    2. Maadili ya watoto (wanafunzi) wakiwa shule na nyumbani ( The effects of globalization)
    3. Maadili ya mwalimu akiwa kazini.
    4.Sera, mahusiano ya mwl. na mwanafunzi inasemaje.? Mf. matumizi ya viboko.
    I have a some detail to talk on each point. Iknow hata ikatokea shule zato zikaboreshwa kuwa gorofa, maabala za kisasa, mishahara mikubwa zaidi n.k.
    Bado kuna mambo madogo yasiyo hitaji hata milions za pesa na niyamsingi yakafanyika na ndio haswa yanayohitajika kwa sasa katika nchi yetu Tanzania.
    KAWOGO DICKSON 0757166840

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mawazo mazuri yatasaidia kuelewa vizuri wapi pa kurekebisha na wapi tulishindwa kama Taifa. Jazba zinaweza ku-invalidate hata kile tulichofanikiwa kwa vile karibia wote tumesoma humuhumu na tunasomesha wototo wetu humuhumu.

      kama ni mabaliko ya muelekeo wa elimu ni njambo linalokubalika. Kutoka katika ndoto za kuajiriwa na kuelekea uhalisia wa kujiajiri kwa vile soko la ajira lishajaa. Nasisi tuko wengi vyuoni, na tuliohitimu ni wengi pia. Sio kama wakati wa uhuru na miaka ya 90.

      Delete
  3. USISEME NI MAAMUZI YA AJABU KUTOKA NJE YA BUNGE WABUNGE WA UPINZANI KWANI BILA KUTILIA MKAZO NA KUFANYA KWA KUTENDA HAKUNA MTU ANGEJUA KUWA KUNA MADUDU KWENYE ELIMU YA TANZANIA, ULE NI MKAZO WA KILICHOSEMWA KWANI WASINGETOKA WEWE UNGEPATA WAPI MDA WA KUAINISHA ULICHOANDIKA HAPO JUU? SO WAKO SAHIHI WATANZANIA TUNATAKIWA TUWE NA MISIMAMAO TUSIPENDE USHABIKI.

    ReplyDelete
  4. Job Title: Warehouse: Picking(10 Posts), Packing(15Posts), Shipping Supervisors(15 Posts),
    Position Location: Honduras(Central America)
    These skills include learning paperwork, basic packaging skills, and demonstration of an excellent work ethic, ability to grow with the team, communication skills, and ability to follow direction. Excelling in this position will allow for upward mobility within the department.

    Key Responsibilities:
    · General assembly of Nestles Company. This includes building kits, labeling products, folding instruction booklets and assisting other Packaging Associates with product finishing.

    · Set up and operate packaging equipment.
    · Ability to process jobs utilizing less complex equipment – pipettes, shrink wrapping, automated libelers, etc.
    · Conduct in-process quality control inspection of finished goods.
    · Perform calibration and preventative maintenance of packaging equipment.
    · The associate may be asked to undertake a Packaging Technician II skill set, which enables their upward mobility.
    Minimum Requirements/Qualifications:
    · Secondary Education and above
    Applicants from African countries are invited to apply
    Individual should be able to handle working in a fast paced environment.
    - Must be able to work within a team towards common goals
    - Must be able to work independently
    Basic mechanical aptitude.
    Ability to work a variety of environments.

    - Must be able to work within controlled environment (clean room, etc).
    · Good communication skills.
    · Basic Knowledge of the metric system.
    · Ability to multitask – organize/process several jobs at once.
    · Ability to wear Personal Protective Equipment when required.

    For applications and information please contact
    Email: jobs@nestles.org

    ReplyDelete
    Replies
    1. UNG'ENG'E TUPU. TUTAFRIE BWANA! MATOKEO YA SIASA KUINGILIA ASASI YA ELIMU NI MABAYA MNO! HATA WASIO WATAALAMU WA ELIMU WANATAKA KUINGILIA MIJADALA YA ELIMU.MIFANO ITOLEWAYO HAINA UTAFITI, HAINA UELEWA WA KINA KUHUSU MATATIZO YA ELIMU YA NCHI NYINGINE UKILINGANISHA NA NCHI YETU.

      Delete
  5. Jamani tuache kuamini kuwa kila kitu kinahitaji kupingwa, nasema hivyo kwn nimeona wabunge wapinzani wanaamini kuwa upinzani ni kupinga kila kitu!!!! lakini sio, kwani watu wote ktk nchi hii tumesoma kwa hiyo miataala inayosemekana ni mibovu japo sio kweli, lakini elimu ya zamani ilikuwa safi, mtu alikuwa akimaliza elimu ya chuo kikuu alikuwa na uwezo wa kuwa mmbunifu wa vitu mbalimbali vinavyoweza kuleta manufaa ktk nchi yetu.
    Elimu imeanza kuyumba miaka ya hivi karibuni, hivyo tunatakiwa kuangalia sababu hasa na sio mitaala kuwa ndio sababu.UNAMLIPA MWL. HELA ISIYOKIDHI MAHITAJI YAKE UNATEGEMEA ATAFUNDISHA KWA MOYO MMOJA KWELI?????? JAMANI WE HAVE TO LOOK VERY IN THIS SECTA!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete