11 February 2013

Jitihada zinahitajika kukomesha wizi wa dawa za Serikali



TATIZO la baadhi ya watumushi wa sekta ya afya wasio waadilifu kuuza dawa baridi katika maduka yao au kuziuza kwa wamiliki wa maduka hayo, bado halijapatiwa ufumbuzi wa kuduma.


Hali hiyo inachangia tatizo la uhaba wa dawa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizopo chini ya Serikali na kusababisha kero kubwa kwa wananchi hasa wa kipato cha chini wasioweze kumudu
gharama za dawa wanazohitaji katika maduka binafsi.

Mwishoni mwa wiki, Rais Jakaya Kikwete aliiagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ishirikiane na Bohari ya Dawa nchini (MSD), kuwasaka watumishi wa sekta hiyo wanaouza dawa za Serikali
katika maduka yao ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Rais Kikwete alisema, Serikali inatambua uwepo wa tatizo la uhaba wa dawa vifaa tiba katika hospitali za Serikali lakini anafahamu dawa zinazopaswa kupelekwa huko, zinaishia kuuzwa au watumishi wa sekta hiyo kuziweka katika maduka yao.

Aliwaonya watumishi wa sekta hiyo na watu wengine waache mchezo huo mara moja kwani kama watabainika kufanya hivyo
na kukamatwa, hatawavumilia au kuwaonea huruma.

Sisi tunasema kuwa, tatizo hili linaigusa jamii kubwa ambayo
tayari imeanza kupoteza imani na Serikali kutokana na sekta
hiyo kukabiliwa na changamoto nyingi ambazo ni kikwazo
kwa wananchi kupata huduma bora za afya.

Tatizo la wizi wa dawa za Serikali, halijaanza jana wal juzi bali
lipo muda mrefu na watumishi waliokutwa na dawa husika katika
maduka yao, hawajachukuliwa hatua zozote ili iwe fundisho kwa
wengine wenye tabia kama hiyo.

Imani yetu ni kwamba, ili tatizo hili liweze kupatiwa ufumbuzi wa kudumu upo umuhimu mkubwa Serikali kufanya operesheni maalumu ya kukagua maduka ya watumishi wa sekta hii ili
kujiridhisha kama dawa wanazouza si za Serikali.

Hatua nyingine ni kushirikisha watumishi wenyewe wa sekta ya afya na wannchi kuwataka watu wanaohusika na biashara ya dawa hizo ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua ambazo pengine zitasaidia kupunguza tatizo lililopo lakini si kulimaliza kabisa.

Ukweli ni kwamba, mtandao unaohusika na biashara hizo ni mkubwa na tayari umeshaona matunda ya kufanya wizi huo
hivyo njia pekee ya kukomesha biashara hiyo ni kuwafunga
wahusika magerezani na kutaifisha dawa zote zilizopo
katika maduka yao ili iwe fundisho kwa wengine.

Kimsingi tatizo linaloisumbua nchi yetu ni utekelezaji wa sheria
na utendaji kazi wa vitendo vinavyohusika kuzuia bviashara za
aina hiyo kutokuwa wabunifu wa kujua ni mbinu gazi watumie
kuzuia uhalifu unaochangia kudhoofisha afya za Watanzania.

Hivi karibuni, kumetokea tatizo la uhaba mkubwa wa chanjo ya pepopunda kwa wanawake wajawazito katika hospitali na vituo
vya afya ambapo hali hiyo imechangia baadhi ya hospitali,
kutoa chanjo hiyo kwa fedha wakati zinatolewa bure.

Umefika wakati wa Serikali kuhakikisha inatembea juu ya maneno yake ili kuboresha afya za Watanzania waliokichagua chama tawala kiwaongoze na kuhakikisha wananchi wanapewa huduma zote za msingi wawe na afya njema ya kukuza uchumi na kujiletea maendeleo.

No comments:

Post a Comment