27 February 2013

Jela miaka 30 kwa unyang'anyiNa Lilian Justice, Morogoro

MKAZI wa Turiani, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro,
Bw. Godluck  Mongi (36), amehukumiwa kifungo cha miaka
(30), jela baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani humo
kumtia hatiani kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.


Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Saraphina Nsana ambapo Mwendesha Mashtaka wa polisi, Anganile Nsyani alidai kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Turiani Machi 4,2011.

Alidai mshitakiwa huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria, alitumia panga kumtishia mmiliki wa pikipiki aina ya Fekon,
Bw. John Charles na kufanikia kuiiba.

Mshtakiwa aliyakana mashtaka aliyosomewa hivyo upande
wa mashitaka ulilazimika kupeleka mashahidi wannne.

Hakimu Nsana alidai ushahidi uliotolewa mahakamani hapo haukuacha shaka kwa mahakama kumtia hatiani mshtakiwa.

Hata hivyo, mshtakiwa alipotakiwa kujitetea aliiomba mahakama, impunguzie adhabu na kudai amekaa muda mrefu gerezani wakati kesi yake ikiendelea kusikilizwa lakini ombi lake lilitupwa.


No comments:

Post a Comment